JAVU AANZA KAZI YANGA
Mshambuliaji mpya wa timu ya Yanga Hussein Javu
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji Hussein
Javu kutoka timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani - Morogoro ambapo
mchezaji huyo leo ameanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari
Loyola Mabibo jijini Dar es salaam.
Usajili wa Javu unafikisha idadi ya washambuliaji sita mpaka sasa
wakiwemo Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Said Bahanuzi, Shaban Kondo
(mpya - Msumbiji) na Realintus Lusajo (mpya kutoka Machava FC - Moshi).
Kikosi
cha mholanzi Ernie Brandts kinaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu
mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza agosti 24 kwa kufungua
dimba na timu ya Ashanti United iliyopanda msimu huu.
Agosti
17-2013 Young Africans itacheza mchezo wa Ngao ya Hisani na timu ya
Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya
ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu kwa msimu wa 2013/2014.
Mpaka sasa klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji saba (7) wapya ambao ni:
1. Deogratius Munishi 'Dida' - Huru Azam FC (Golikipa)
2.Rajab Zahir - Huru Mtibwa Sugar (Mlinzi wa kati)
3.Hamis Thabit - Huru Ureno (Kiungo)
4.Shaban Kondo - Huru Msumbuji (Mshambuliaji)
5.Mrisho Ngassa - Huru Azam FC (Kiungo mshambuliaji)
6.Reanlintus Lusajo - Huru Machava FC (mshambuliaji)
7. Hussein Javu - Mtibwa Sugar (mshambuliaji)
Kikosi
kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kila
siku saa 2 asubuhi na wachezaji waliopo katika timu ya Taifa Tanzania
(Taifa Stars) wanatarajiwa kuungana na wenzao katika mazoezi siku ya
jumatatu.
chanzo na http://www.youngafricans.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA