NEC yatangaza uchaguzi kata 27 kufanyika mwezi February mwakani
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo
wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza
sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani. Akizungumza
na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema
uchaguzi huo utafanyika katika halmashauri 23 baada ya kukamilisha
taratibu zinazotakiwa.
Alizitaja kata hizo na halmashauri zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).
Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti
(Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba),
Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na
Namikago (Nachingwea).
Kata nyingine ni Partimbo na Loolera
(Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga),
Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini
(Njombe) na Nyasura (Bunda).
Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati
kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya
kupiga kura itakuwa Februari 9.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA