Mkurugenzi
wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni
atashiriki warsha ya wakufunzi wa makocha wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika kuanzia Oktoba 22-24 mwaka huu.
Warsha
hiyo iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya wakufunzi wake itafanyika nchini
Cameroon. Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa makocha watahudhuria warsha
hiyo.
Madhumuni
ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao, kubadilishana uzoefu. Pia
kuwapa methodolojia mpya ya ufundishaji na muongozo kuhusu mfumo wa
leseni za makocha ambao watautumia katika nchi wanazotoka.
Mbali
ya Kayuni Tanzania, wakufunzi wengine ni Ahmed Babiker (Sudan), Amadou
Shaibu (Nigeria), Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu Fred Osam
(Ghana), Edussei Anthony (Ghana), Fathi Nossir (Misri), Faouzy Altaisha
(Sudan) na Fran Hilton Smith (Afrika Kusini).
Wengine
ni Francis Oti-Akenteng (Ghana), Honour Janza (Zambia), Kasimawo Laloko
(Nigeria), Mahmoud Saad (Misri), Paul Hamilton (Nigeria), Serame
Letsoaka (Afrika Kusini), Shawky Abdel Shafy (Misri), Thondoo Govinder
(Mauritius) na Ulric Mathiot (Seychelles),
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
1 Weka maoni yako hapa:
HANA LOLOTE LILE
Post a Comment
COMMENT HAPA