Mashindano
ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame)
yanayoandaliwa na Baraza la Vyama ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA) yatafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-29 mwaka
huu ambapo timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Juni 25
mwaka huu.
Yanga
itashiriki mashindano hayo ikiwa bingwa mtetezi, wakati Tanzania Bara
itawakilishwa na mabingwa wake Simba na Makamu bingwa Azam. Mashindano
hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa na Uwanja
wa Chamazi pekee kwa sababu ya kupunguza gharama za uendeshaji.
Ratiba
ya mashindano hayo yanayoshirikisha mabingwa kutoka nchi kumi na moja
ambao ni wanachama wa CECAFA itapangwa Juni 29 mwaka huu.
Mashindano
haya ni muhimu kwa CECAFA na Tanzania Bara ambayo ndiyo mwenyeji kwa
maendeleo ya mpira wa miguu na pia kukuza kiwango cha mchezo huo kwa
ukanda huu ambao kwa Afrika unaoongoza kwa kufanya mashindano mengi ya
timu za Taifa pamoja na klabu.
Mwenyekiti
wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Leodegar Tenga amewaomba wadau kujitokeza kudhamini michuano hiyo
ambayo itaoneshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport. Pia
amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuunga mkono michuano
hiyo.
CECAFA
inawashukuru wadau wote kwa kuwezesha michuano hiyo kufanikiwa akiwemo
Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa kutoa zawadi za fedha kwa washindi,
Serikali ya Tanzania kwa kutoa Uwanja wa Taifa na Kamati ya Utendaji ya
TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Mjumbe, Kamati ya Habari CECAFA
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA