Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kulia) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh.
Milioni 20, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa (kushoto) katika hafla
fupi ya kukabidhi hundi hiyo iliyofanyika makao makuu ya TBL, Ilala Dar es
Salaam asubuhi ya leo.
TBL imetoa fedha hizo kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa klabu
hiyo, uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,
Julai 15, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa udhamini baina ya Yanga na
Kilimanjro Premium Lager Beer, inayozalishwa na TB L.
Wengine nyuma yao, kutoka kulia ni Katibu wa Kamati ya
Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili, Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Angetile Osiah, Meneja wa Bia ya Safari Lager aliyemuwakilisha George Kavishe, Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro aliye safarini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Yanga, Jaji John Mkwawa.
|
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA