Kikosi cha pili cha mabingwa wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati, Dar
Young Africans kinachojiandaa na michuano ya Rollingstone kimekubali
kufungwa goli 3-2 na Jamhuri ya Pemba, katika mchezo wa kombe la urafiki
uliokwisha hivi punde.
Katika mchezo huo Yanga walikuwa wa mwanza kupata goli katika dakika ya 18 mfungaji akiwa Shaban Hamisi.
Jamhuri walifanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 34, na
kuongeza jingine katika dakika ya 45. Hivyo kupelekea Yanga kwenda
mapumzika wakiwa nyuma kwa goli 2-1.
Katika dakika ya 69 Jamhuri walifanikiwa kuandika goli la tatu huku
Yanga wakifunga goli lao la pili katika dakika ya 77 kupitia kwa
Notekelly Masasi, na kupelekea mpira kumalizika kwa Yanga kufungwa goli
3-2.
Habari kwa niaba ya
http://aboodmsuni.blogspot.com/ wa SPORTS IN BONGO
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA