Azam FC haiachi walio na mikataba na haiongezi mchezaji mpya
Kama ilivyokuwa wakati wa dirisha kubwa la usajili 2012/13 ambapo Azam
FC ilimuongeza George Odhiambo Blackberry pekee, safari hii tena Azam FC
imeamua kwapandisha wachezaji wawili wa Under 20, Mudathir Yahaya na
golikipa Hamadi Juma Yahya Kadedi na kufunga zoezi la usajili.
Kwa mujibu wa ripoti toka kwa Kocha mkuu wa Azam FC mtaalam Stewart
Hall, hakuna sababu ya klabu kwenda nje kusajili wachezaji ambao
viwango vyao havipishani na waliopo klabuni.
Mchezaji Abdulhalim Humoud amepata timu nchini Afrika ya Kusini, Abdi
Kassim Sadala Babi mkataba wake umekwisha kama ilivyo kwa Deogratius
Munishi Dida huku Uhuru Selemani akirejeshwa Simba SC baada ya kumaliza
msimu wa mkopo na Azam FC.
Wachezaji wengine wote waliosalia
wanabaki klabuni na kocha mkuu amependekeza baadhi ya makinda wa Under
20 walioonesha viwango vya juu wapandishwe timu kubwa, wapewe mikataba
na kisha wapelekwe kwa mkopo ili wakapate nafasi ya kucheza. Wachezaji
hao ni Omary Mtaki na Kevin Friday.
Azam FC ambayo imemaliza
ligi ikishika nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo itaanza kambi
ya kujiandaa na msimu mpya hapo June 24 kwa mujibu wa ratiba ya mwalimu
na baada ya kumaliza kipindi cha pre season, kikosi cha Azam FC
kitasafiri nje ya nchi kucheza mechi za majaribio kama ilivyo kawaida
yake.
Wachezaji wanaounda kikosi cha Azam FC ni
Magolikipa; Mwadili Ally, Aishi Salum na Hamad Juma Yahya
Mabeki; Himid Mao, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samih Nuhu, Luckson
Kakolaki, Aggrey Morris, Said Moradi, David Mwantika na Jockins Atudo
Viungo; Kipre Bolou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Humphrey Mieno na Mudathir Yahya
Washabuliaji; John Bocco, Gaudence Mwaikimba, Khamis Mcha, Kipre Tchetche, Brian Umony na Abdallah Seif Karihe
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA