Timu ya Real Madrid imesema macho yao yako kwa Luka Modric na wako tayari kubadilishana na Mfaransa Lassana Diarra na pesa kiasi cha paund million 22 Diarra ambae sasa ni muda mrefu amekuwa hayuko katika kikossi cha kwanza cha kocha Jose.
Hata napo Chelsea nao wanaonesha nia ya kumtaka Luka Modric tajiri wa Chelsea Roman Abromovich amesema baada ya kutimiza ndoto yake ya kuchukua ubingwa wa club bingwa Ulaya sasa wanataka kutengeneza kikosi chao na kuwa imara msimu ujao na miongoni wa wachezaji wanaowataka ni pamoja na Hazard na Falcao
Wakati Chelsea wakijianda na usajili mshambuliaji wa timu hiyo Didie Drogba amesema kama hata pata mkataba wa miaka miwili basi atakenda kucheza soka nnchini China .
Swali lililobakia kwa chelsea ni kama itabaki na kocha wake wa sasa Di Matteo maana kocha huyu sio chaguo la kwanza la bodi ya Chelsea na chaguo lao lilikuwa kwa na hata kwa tajiri wao lilikuwa ni Pep Guardiola hata napo Pep Guardiola amesema anayaheshimu maamuzi yake ya kupumzika mwaka mmoja na si pesa wala nini kinachoweza badilisha maamuzi yake
Didie Drogba akiwa ameshikilia kombe la klab bingwa Ulaya
Lille's Hazard chaguo la Chelsea
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA