MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA
*Polisi waokoa Tzs 800 milioni
*SMG na Gobole vyapatikana
Ujambazi wa kutisha umetokea leo asubuhi maeneo ya Uwanja wa Taifa karibu na zilipo Ofisi za BMT ambapo Majambazi wawili
wameuawa.
Majambazi hao ambao majina yao hayakufahamika waliuawa papo hapo wakati walipokuwa wakijibizana kurushiana risasi na Polisi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichokuwa eneo la tukio
kinasema Polisi walikuwa na taarifa za kufanyika kwa tukio la ujambazi walizopewa na msamaria mwema (jina kapuni) siku mbili kabla.
Majambazi hao bila kujua kama tayari wamewekewa mtego na Polisi ambao wapo makini na kazi yao, wakaingia mzigoni kwa lengo la kupora fedha zinazokadiriwa kufikia Tzs 800 milioni mali ya Kampuni inayojishughulisha na Ujenzi wa Uwanja wa Taifa.
Fedha hizo zilizopona kuporwa zilitengwa kwa ajili ya mishahara ya
wafanyakazi, vibarua na manunuzi ya vifaa.
Wananchi wengi wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa uhodari waliouonesha katika kupambana na majambazi wale na bila kuvujisha SIRI.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA