Oct 4, 2022

MEYA KINONDONI AWATAKA WATANZANIA KUFANYA MAZOEZI TIBA

 


Meya Kinondoni  Awataka Watanzania  Kufanya Mazoezi tiba.

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Songoro Mnonge ameiasa Jamii ya Kitanzania kuwa na desturi ya kufanya mazoezi  tiba angalau mara moja kwa wiki kwa manufaa yako mwenyewe.

Songoro aliyasema hayo alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Mazoezi tiba ya Kisiwani Clinic Centre(KCC) yenye makazi yake Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam ambayo sherehe zake za kutimiza mwaka mmoja zilifanyika mwishoni mwa wiki Viwanja vya CCM ,Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam.

Songoro aliipongeza KCC kwa juhudi inazozifanya za kusaidia jamii kwani wanaisadia Serikali kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukizwa na Serikali imeliona hili.

Aidha Meya Songoro alimuomba Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ambaye pia alihudhuria sherehe hizo kuwa mwakani watenge bajeti ya shughuli zinazofanywa na jamii kwa kujitolea kama hizi naye kama Meya atazisimamia kuhakikisha zinapitishwa kwa maufaa ya jamii badala ya vikundi kuchangishana.

Songoro alimaliza kwa kuwapongeza KCC kwa kazi kubwa waliyoifanya  ya kukusanya umati mkubwa wa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi tiba na kuimba jamii basi ihamasike kweli kwani kauli mbiu ya maadhimisho haya kila mmoja inamhamasisha kweli afanye mazoezi kwani ni dhahili “Afya yako mtaji wako” ni kauli mbiu nzuri bila afya bora huwezi kuwa na manufaa kwa jambo lolote kwenye familia yako mpaka jamii inayokuzunguka.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni alitoa shukrani kwa taasisi ya kujitolea ya KCC kwa kazi kubwa ya kukuzanya umati wa zaidi ya 2000 kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kwa kauli mbiu ya “Afya yako Mtaji wako”

Pili aliahidi kushirikiana na KCC pamoja na vikundi vingine vya kusaidia jamii vyenye mlen go kama KCC Daima katika zoezi dhima la kuisaidia jamii kuondokana ama kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.

Laiza alimaliza kwa kuahidi kushirikiana na Taasisi kwa kuwakilisha bajeti za vikundi kama KCC ili kupunguza maumivu ya vikundi kuchangishana ili kufanya hamasa ya kusaidia jamii ifanye mazoezi kwani tutakuwa tunaisaidia Serikali kufunguza Madawa ya kuhudumia Wagonjwa kadhaa wa magonjwa yasiyoambuza.

Nae mratibu wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mmoja wa KCC, Michael Machela  alishukuru kwa shughuli zote kufanyika kwa usalama na kwa kufana , ambapo maadhimisho yalihudhuliwa na vikundi vya Jogging 43 vyenye idadi ya Wanachama 25 mpaka 35 kila kikundi.

Lakini pia kulikuwa na Wananchi ambao walifuata huduma za matibabu mbalimbali zilizoalikwa katika maadhimishi hayo ambapo kulikuwa na JK Muhimbili ambao walikuwa wanatoa huduma za Magonjwa ya Moyo, Ocean Road wenyewe walikuja na huduma ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa kina Mama, Saratani ya Matiti kwa kina Mama na Saratani ya Tezi Dumea kwakina Wanaume, KAM wenyewe walikuja na huduma ya Kinywa na Manispa ya Kinondoni kupitia Hospitali ya Magomeni na Mwananyamala walikuja na huduma ya Macho, Sukari, Shinikizo la damu, kupima uzito, kuchangia damu pamoja na ushauri wa kitaalamu.

Kwa ujumla maadhimisho ya Kisiwani Clinic Centre yalihudhuliwa na Watanzania zaidi ya 2500 kutoka kona zote za jiji la Dar es Salaam.


0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA