TBL YAKABIDHI VIFAA
Kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Baraka
Kizuguto , Geofrey Makau na Lawrence Mwalusako Katibu Mkuu wa Yanga
wakionyesha vifaa walivyokabidhiwa na kampuni ya bia nchini TBL
Wadhamini wa klabu ya Young Africans
Sports Club kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro leo
imekabidhi vifaa kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati maarufu kama kombe la Kagame inayotazamiwa kuanza Juni
18 mwaka huu nchini
Sudan.Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
George Kavishe alisema, ‘‘ Bila ubishi Yanga na Simba ndio klabu kubwa
za mpira Tanzania na zote zimefika katika fainali za mchuano wa Kombe
la Kagame kwa mara ya 19 sasa, haya ni mafanikio makubwa kwa hizi timu,
kama wadhamini wakuu wa timu hizi, Kilimanjaro Premium Lager inaziunga
mkono Simba na Yanga katika harakati zao kucheza tena fainali za
michuano hii ya kusisimua na ya kihistoria.
Aliongeza kuwa Kombe
la Kagame ni mashindano makubwa Africa mashariki na kati, na ni jukwaa
bora kwa wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao dhidi ya wachezaji wa
viwango vya juu katika kanda hii lakini pia ni jukwaa zuri kwa wale
wanaounda timu za taifa kuchagua wachezaji.“Ushirikiano huu baina
ya Bia ya Kilimanjaro na klabu hizi ni mizizi inayotokana na maadili
katika kazi, kufanya kazi kama timu na ile kiu ya mafanikio.
Na
mafanikio ya ushirikiano huu ni pamoja na kushuhudia mara kwa mara timu
hizi mbili zikitoa wachezaji kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ambao
wamekuwa na matokeo mazuri chini ya udhamini wa Bia ya Kilimanjaro.
Tutaendelea kusaidia timu hizi, na kuhakikisha tunapeleka mpira wa nchi hii kwenye kilele cha mafanikio.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro pia aliwataka Simba na Yanga kuhakikisha
wanaiwakilisha nchi yetu vizuri katika mchuano huu mkubwa wa vilabu
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kuwasihi kuchukua ushindi
na kurudi na kombe la 12 la Kagame kwa mashabiki wanaosubiria kwa hamu
Akiongea
kwa niaba ya klabu ya Yanga, Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako
aliwashukuru TBL kupitia kinywaji chake cha Kilmanjaro kwa udhamini
wanaoutoa kwa timu yake, kwani wanajivunia kuwa na wadhamini bora ambao
wanawafanya kuweza kufanya vizuri katika michezo na kuahid kuendeleza
kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA