BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA
Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa
Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia
takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo Gospel Kitaa imezipata kutoka
kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola
amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo
Slipway jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na
maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India
kwa matibabu.
Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.
kwa hisani ya http://gospelkitaa.blogspot.com