Sep 20, 2013

HUYU NDIO HAKIMU ALIYOSHAMBULIWA BAADA YA KUTOA HUKUMU HAPO JANA

Hakimu wa mahakama ya mwanzo mkoani Shinyanga achomwa kisu na mlalamikaji baadaya ya kutoa hukumu kwa mtuhumiwa,hakimu huyo alitoa hukumu kwa mtuhumiwa wa wizi wa baiskeli yenye thamani ya 150000 aina ya neria,hukumu hiyo alitoa ikiwa mtuhumiwa hayupo mahakamani mala tu baada ya kutoa hukumu hiyo mlalamikaji aliwashukuru mahakama kwa uamuzi huo kisha akatoka nje baadaye akaingia ofisini kwa hakimu kwa kigezo cha kwamba alisahau kumpatia risti alyonunulia baiskeli baada ya muda kidogo alipoingia alianza kumshambilia hakimu kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za, mwili wake na baadaya akakamatwa na jeshi la polisi na kisha hakimu kukimbizwa hospitari ya mkoa wa Shinyanga.
HAKIMU ASHAMBULIWA KWA KISU BAADA YA KUTOA HUKUMU 


HAKIMU AKIPATIWA MATIBABU

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.

Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.

Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.

Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.

Hata hivyo, baada ya kutoa maelezo, si mshtakiwa wala mdhamini wake aliyehudhuria mahakamani hapo licha ya kesi hiyo kusikilizwa mara mbili bila ya taarifa yoyote kabla ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo jana.

Kushambuliwa

Baada ya hukumu hiyo mlalamikaji alitoa shukrani na kuwashika mikono wote waliokuwamo mahakamani humo na kutoka nje.

Ilidaiwa kuwa baada ya dakika 15, Izengo alirudi mahakamani hapo na kudai kuwa ameleta risiti ya kumwonyesha hakimu thamani ya baiskeli yake alipoingia ndani ndipo kelele za Mshauri wa Baraza, Mary Wamba zikaanza kusikika akisema: ‘Njooni jamani hakimu kavamiwa anapigwa’.

Baada ya watu waliokuwa karibu kuingia katika ofisi ya Mahakama hiyo walikuta hakimu ameshacwhomwa kisu katika shavu la upande wa kushoto huku akivuja damu nyingi huku mtuhumiwa huyo akiendelea kumshambulia. Baada ya tukio hilo, wasamaria wema walimpeleka hakimu huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema mtuhumiwa alikamatwa mara baada ya tukio hilo kusubiri hatua za kisheria dhidi yake.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA