Mstahiki Meya wa Manisapaa ya Ilala Jerry Slaa akisaini kupokea barua
kutoka klabu ya Yanga, kulia ni mwenyekiti wa mipango na makazi wa
manispaa ya Ilala Sultan Salum
Meya wa Manisapaa ya Ilala jijini Dar es salaam mstahiki Jerry Slaa
leo amepokea maombi ya klabu ya Young Africans kuhusu kuomba eneo la
ziada kwa ajili ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa uwanja wa kisasa
eneo la Jangwani.
Mara baada ya kupokea barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya
wadhamani wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe, Slaa alisema yeye pamoja na
wenzake hawaoni sababu ya kuzuia harakati hizo za maendeleo na faida
kwa wanachi wa mkoa wa Dar es salaam.
"Kwanza viongozi wa Yanga
poleni sana kwa kuchelewa kufika, nilikuwa nawasubira wenzangu naibu
meya pamoja na mwenyekiti wa mipango na makazi wa manispaa ili tuje
kuonana na nyie pamoja, kwa kifupi suala lenu litafanyiwa kazi na
kufikia mwezi ujao Novemba tayari tutakua tumeshawapatia majibu" alisema
Slaa.
Wazee wangu, wanachama pamoja na viongozi suala hili
nalikabidhi kwa mwenyekiti wa mipango ili aliwasilishe kwenye kikao cha
madiwani na kufikia mwezi ujao tayari majibu yatakua yameshapatikana ili
muweze kuendelea na mchakato huo wa maendeleo kwa watanzania.
Akisoma
maelezo ya barua mwenyekiti wa bodi ya wadhamini alisema, tumeshangoea
na watu wa mazingira na wamemsea wapo tayari kusaidiana na sisi ila
kikubwa ni tulikua tunasubiri majibu kutoka manispaa ya Ilala juu ya
eneo la ziada tulioliomba.
Mara baada ya kikao hicho cha pamoja
katibu wa baraza la wazee mzee Ibrahim Akilimali alitoa shukrani kwa
mstahiki meya pamoja wasaidizi wake kwa kuweza kukutana na viongozi wa
Yanga na kuweza ahadi ya kulimaliza suala lao la eneo la ziada haraka
iwezekavyo
CHANZO NA http://www.youngafricans.co.tz
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP 2012
ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi ya
New Bo...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA