Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za
dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni
mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya
vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.
Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne
iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni
mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso)
aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na
vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.
Huyo binti anaitwa Jackie Cliff. ..appeared in Diamondz Nataka Kulewa. Was a runners up or something kwenye Miss Tz huko nyuma.
Polisi wakichunguza vidonge ambavyo huyu mrembo alikuwa amevimeza.
Waandishi wa habari wakipiga picha vidonge vya heroin alivyokamatwa navyo mremboi huyu wa Kitanzania.
CHANZO JAMII FORUM
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP 2012
ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi ya
New Bo...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA