Picha: Mavazi ya 'kisharobaro' ya Mike Sonko yawavunja mbavu rais Uhuru Kenyatta na Ruto
Senator Mike Sonko ambaye amekuwa maarufu kutokana na jinsi
anavyoishi maisha ya ‘kisharobaro’ aliwavunja mbavu rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta na makamu wake Ruto kwa mavazi yake.
Rais Uhuru na Ruto walikuwa uwanja wa ndege wakimpokea kiongozi wa
China, Li Keqiang na walipokuwa uwanjani hapo walikutana na Sonko ambaye
pia alikuja kwa shughuli hiyo.
Uhuru na Ruto walishindwa kujizuia na kuangua kicheko walipomuona
Sonko akiwa amevaa koti zuri la suti na tai huku chini akiwa ametupia
jeans iliyochanwachawa (fashion). Rais Uhuru alionekana kwenye picha
akicheka huku akinyoosha kidole kwenye jeans ya Sonko na Sonko.
na timesfmtz.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA