
Klabu ya Yanga imepongezwa kwa juhudi mbalimbali katika kuendeleza
mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini pamoja na harakati za uhuru wa
Tanzania na Msumbiji.
Wakizungumza wakati wa ziara yao wakati walipotembelea Makao
Makuu ya Klabu ya Yanga Kiongozi wa msafara huo Florinda Mauribe kutoka
Chuo cha Ualimu cha Ajuda do Dusenvolinmento do Povopara O
Povo-Escola
de Professones do Futuro-Chimdio, alisema wamejisikia furaha sana kufika
makao makuu ya klabu ya Yanga, kuona mazingira ya klabu na kupewa
historia fupi ya timu hii kongwe katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Mauribe
amesema Wananchi wa Msumbiji wanathamini mchango mkubwa wa ukombozi wa
nchi yao kwa Tanzania ikiwemo Yanga ambapo wananchi hao wanayo taarifa
kuwa baadhi ya Wapenzi na Mashabiki wa
Yanga walitoa mchango wa hali na
mali katika kusaidia harakati za ukombozi katika nchi hiyo ya Msumbiji.
Wanafunzi
hao walitembezwa katika jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na
kujionea mambo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa Kaunda unaotarajiwa
kufanyiwa matengenezo,Gym ya mazoezi,Bwawa la kuogelea na Mtandao wa
Klabu ya Yanga wa www.youngafricans.co.tz. kwa hisani ya mtanadao wa Yanga sport club
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA