Oct 20, 2013

LEO NDIO LEO NI KATI YA SIMBA NA YANGA

IKIWA YAMEBAKI MASAA MCHACHE TOKA SASA KARIBIA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA KUCHEZWA TAYARI TIKETI ZA 5000 7000 NA 10000 ZIMEKWISHA KATIKA KITUO CHA UWANJA WA TAIFA NA BAADHI YA MAENEO YANAYOUZA TIKETI I.

ILA UKITAKA TIKETI HIZO UTAZIPATA KWA MADALALI KAMA KAWAIDA YA 5000 KWA 7000 NA 7000 KWA 9000 HILI SASA NI TATIZO LA KUDUMU KATIKA SOKA HUSUSANI MECHI KATI YA SIMBA NA YANGA AU YANGA NA AZAM. 

MARA NYINGI WATU WAMEKUWA WAKIKOSA NAFASI YA KUONA MPIRA KUTOKANA NA WAJANJA WACHACHE AMBAO HUNUNUA TIKETI ZOTE NA KUANZA KUUZA WAO NA BAADI YA WENYE DHAMANA YA KUUZA TIKETI KUWAPA NDUGU ZAO AU JAMAA ZAO KWA LENGO LA KUPATA FAIDA

PIA LEO USISHANGAE UNAINGIA MLANGONI TIKETI YAKO ISICHANWE NA UKAPEWA KIPANDE KINGINE KISHA TIKETI YAKO IKARUDI  NJE NA KUUZWA TENA .

MAONI TFF IWEKE UTARATIBU WA TIKETI KUUZWA SIKU YA MECHI TENA KWA WAO KUKAA KWA NDANI NA WANUNUZI KWA NJEE KWANI UWANJA WA TAIFA UNAENEO AMBALO TIKETI ZINAWEZA KUUZWA NA WATU KINGIA UWANJANI BILA TABU HUKU TUKISUBILI TIKETI ZA MASHINE.


 MASHABIKI WA YANGA

MASHABIKI WA SIMBA

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA