Apr 27, 2013

Al-Shabaab yalengwa na sheria ya Somalia ya kupambana na ugaidi

Katika siku zijazo bunge la Somalia litajadili pendekezo la sheria dhidi ya ugaidi ambayo inawalenga al-Shabaab na inalenga kurekebisha usalama wa taifa wa nchi na huduma za usalama katika kupambana dhidi ya ugaidi. 

 Magari yakiungua baada ya walipuaji bomu wa kujitoa mhanga wa al-Shabaab kushambulia majengo ya mahakama kuu ya mkoa yaliyopo Benadir mjini Mogadishu tarehe 14 Aprili, 2013. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]
 Magari yakiungua baada ya walipuaji bomu wa kujitoa mhanga wa al-Shabaab kushambulia majengo ya mahakama kuu ya mkoa yaliyopo Benadir mjini Mogadishu tarehe 14 Aprili, 2013. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]
Baraza la mawaziri la Somalia lilipitisha mswada wa sheria ya kupambana na ugaidi tarehe 18 Aprili, siku nne baada ya operesheni ya al-Shabaab kuua kiasi cha raia 29 wakati wa uvamizi wao katika majengo ya mahakama kuu ya mkoa wa Benadir.

Maelezo kwa urefu ya mapendekezo ya sheria bado hayajatolewa kwa umma, lakini itapatikana mara baada ya majadiliano kuanza bungeni.

"Hiki ni kipande muhimu sana cha sheria ambacho kinawakilisha kiungo muhimu katika mkakati wa serikali wa kupambana na ugaidi kwa upana wakati ikichukua dhamana ya mipaka yetu na usalama wa watu wetu," Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon alisema katika taarifa iliyotayarishwa na kutolewa baada ya mswada kupitishwa.

"Tutaendesha kampeni za kupambana na ugaidi kwa mujibu wa sheria kali, za uwazi na zinazoaminika ambazo zina imani ya umma wa Somalia na ambazo zinaheshimu kikamilifu haki za binadamu za kimataifa," Shirdon alisema baadaye katika mfululizo wa ujumbe zilizotumwa katika akaunti yake ya Twitter. 

"Tuko katika hatua za mwisho za kampeni za kijeshi dhidi ya adui ambaye amebakia kuwa kufanya ugaidi na operesheni za vita vya msituni," alisema.

Kuwaadhibu magaidi

Mswada wa sheria dhidi ya ugaidi ni sehemu ya mkakati wa serikali ya shirikisho wa kupambana na vikundi vya wapiganaji wanaojaribu kuidhoofisha nchi, Naibu Waziri wa Habari, Posta na Mawasiliano ya Simu Ibrahim Isaaq Yaroow, alisema.

"Nchini Somalia, tunahitaji kwa haraka sana sheria kama hiyo, ambayo inafanya kuwa rahisi kumaliza hatari ya magaidi ambao wanatishia usalama wa nchi na kuhatarisha jamii na taifa," aliiambia Sabahi.

"Sheria mpya inajumuisha vipengele vingi vilivyotayarishwa maalumu kwa kupambana na ugaidi kama dhana na kuwaaadhibu magaidi ambao wanawatisha na kuwaua wananchi wasio na hatia," alisema. "Sheria mpya imekuwa muhimu sana kutokana na hali ya sasa ya usalama, kwa hivyo tunatumai kuwa bunge litaipitisha sheria hii kwa haraka iwezekanavyo." 

Hassan Abdirahman, aliyekuwa mshauri wa Wizara ya Sheria, alisema kuwa mapendekezo ya sheria dhidi ya ugaidi yanaimarisha usalama na utulivu wa taifa la Somalia. Aliitaka serikali kutumia hatua zote ilizonazo ili kupambana na ugaidi. 

"Hakuna nchi inayoweza kuwepo wakati inatishiwa kutoka ndani na Somalia ni nchi yenye vitisho vya ndani kutokana na matokeo ya ugonjwa unaoitwa ugaidi," Abdirahman aliiambia Sabahi. "Watu wa Somalia tayari wamechomwa na magaidi ambao wanatishia usalama wa nchi yao." 

Mohamed Hussein, mchambuzi wa masuala ya kisiasa aliyepo Mogadishu, aliipokea sheria ya kupambana na ugaidi lakini akaelezea wasiwasi wake kuhusu iwapo itaathiri uhuru na haki za watu. 

"Somalia inahitaji sheria dhidi ya ugaidi lakini sheria kama hiyo haipaswi kutumika kama kisingizio cha kukiuka haki za msingi na uhuru wa binadamu," Hussein aliiambia Sabahi. "Natumai kuwa bunge la Somalia litaipitia kwa makini sheria hii mpya."

Osman Mohamed Roble, dereva wa taksi wa Mogadishu mwenye umri wa miaka 47, alisema kuwa anatumai kuwa sheria hiyo itasaidia kumaliza operesheni za kigaidi nchini Somalia.

"Nadhani ni hatua muhimu sana kwa sababu tunahitaji sheria ngumu za kuwaadhibu wale wanaohusika na milipuko na operesheni za kujitoa mhanga ambazo zinaua wananchi wasio na hatia," alisema. 

"Wananchi wanapaswa kusimama pamoja ili kupambana na magaidi hawa. Tunapaswa kuvisaidia vikosi vyetu shupavu vya usalama katika vita vyao dhidi ya ugaidi kwa kuvipatia habari za wapi waliko magaidi katika sehemu yoyote ya nchi," alisema.

chanzo na  http://sabahionline.com

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA