Aug 27, 2013

Hatimaye Mansoor Yussuf Himid, mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki mjini Unguja, amekubali kufanya mazungumzo yake ya kwanza na Idhaa ya Kiswahili ya DW tangu uamuzi wa Chama chake cha Mapinduzi wa kumvua uanachama


Kwa mujibu wa taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari ni kwamba Mansoor amevuliwa uwanachama baada ya kukiuka miiko ya chama hicho tawala nchini Tanzania, hasa kwenye suala la muundo wa Muungano. 

Katika mazungumzo haya na Sudi Mnette, kwa mara ya kwanza mwansiasa huyo kijana, ambaye hapo jana Halmashauri Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuza chamani, ameeleza baadhi ya yale yaliyo moyoni mwake. 

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sudi Mnette Mhariri: Mohammed Khelef

KWA SAUTI FUATA HAPO CHINI
 
SAUTI YA MAHOJIANO YAO

CHANZO NA http://www.dw.de