Aug 13, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. KAULI YA KOVA NI YA KUMUHUJUMU RAIS.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
KAULI YA KOVA NI YA KUMUHUJUMU RAIS. 

Kufuatia tamko la Kamanda wa Kanda Maalum wa Mkoa wa Dar es Salaam la kutoa Onyo kwa Waislama na kusema kwamba wanamshikilia Sheikh Ponda kwa tuhuma mbili. 1 . Kutokana na Tukio la Morogoro 2 . Kukiuka Masharti ya Kifungo cha Nje alichohukumiwa mwanzoni mwa Mwaka huu.

CUF-Chama cha Wananchi kinatafsiri tamko hili kama muendelezo wa kile kinachoonekana kuwa ni hujuma dhidi ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 
 Hatuoni sababu ya Kamanda Kova kutoa Onyo kwa Waislam kwa jambo ambalo Waislam wameshatoa tamko kupitia Amiri wao Sheikh Mussa Kundecha na kuiomba Serikali kuunda Huru ya Kuchunguza tukio hilo. Tangu litolewe tamko hilo hakuna Muslam yoyote alifanya jaribio lolote la kutaka kulipa kisasi kwa Polisi au kwa Mtendaji yoyote wa 
Serikali. Sasa kuna haja gani ya kutoa Onyo kwa jambo ambalo Waislam wamesha kubali maelekezo ya Viongozi wao ? Pili kutangaza kumshikilia Ponda akiwa Hospitali ambako anapata Matibabu kwa kisingizio au kwa tuhuma za Tukio la Morogoro au kukiuka masharti ya kifungo cha Nje ni hoja zisizo na mashiko. 
Suala la Morogoro Makao Makuu ya Jeshi la Polisi imeunda Tume ya kuchunguza tukio hilo, na tayari tume imeshaanza kazi ya kukusanya Taarifa kwa Watu mbali mbali Mjini Morogoro. Sasa wewe Kamanda wa Kanda Maalum unahusikaje kwenye jambo hilo la Morogoro ? 
Au umepewa maagizo ya kumkamata Ponda na Tume ilioundwa toka Makao Makuu ? Iwapo umepewa Amri, je Tume hiyo imeshakabidhi ripoti yake kwa IGP Saidi Mwema na imependekeza Ponda akamatwe kwa tukio hilo kwamba yeye ndi muhusika alimpiga risasi Sheikh Ponda ? (Hapa nina maana amejipiga risasi mwenyewe ? ) 
Hivi Kova ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ? Suala la kukiuka Masharti ya Kifungo cha Nje, hivi Kova unayafahamu hayo masharti na umepata agizo lolote toka kwa Haakimu au Mahaka ilimuhukumu Sheikh Ponda ,kwamba umkamate kwa kuwa amekiuka Mashari ? 
Maswali yote haya , yanakupa majibu na mtazamo sahihi kwamba Kova unafanyakazi ya kumuhujumu Rais. CUF-Chama cha Wananchi kinaitafsiri kauli ya Kamanda Kova kama imelenga kutoboa Jahazi lililobeba hasira za Waislam katika suala hili la kupigwa risasi Sheikh Ponda. 
Kauli hii inapaswa kulaaniwa na wapenda Amani wote. CUF-Chama cha Wananchi kinamshauri Kamanda Kova kwa sio lazima kujibu kila jambo unaloulizwa na Waandishi wa Habari, na ikiwa lazima kujibu, basi uwe na mapimo ya kile unachojibu kwa maslahi ya Nchi na usijibu tu kwa maslahi yako.
 Mwisho kabisa CUF-Chama cha Wananchi kinamtaka IGP Kutoa ufafanuzi juu ya kauli tata za Kamanda Kova.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA