Lawrence Mwalusako katibu mkuu
Uongozi wa klabu ya Yanga umeahirisha mkutano wa dharura wa
wanachama wote uliokuwa ufanyike siku ya jumapili tarehe 18.08.2013
katika viwanja vya sabasaba ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam saa 3:30
asubuhi kujadailiana juu ya suala la Azam TV kurusha michezo yake.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu
kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa Yanga, katibu mkuu wa Yanga Lawrence
Mwalusako amesema mkutano huo umeahirishwa kufuatia kuwepo kwa kikao
kati ya Naibu Waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo mhe. Amos
Makalla na viongozi wa kamati ya Ligi, TFF, Azam Media na viongozi wa
klabu ya Yanga.
Ifuatayo ni taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
Ikumbukwe
kuwa hivi karibuni , uongozi wa Yanga uliitisha mkutano Mkuu wa dharura
uliokuwa ufanyike tarehe 18 Agost 2013 viwanja vya sabasaba kwenye
ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la kujadiliana na suala la Azam
Television kurusha mechi za Yanga. Mkutano huo kwa sasa umeahirishwa
kutokana na sababu ifuatayo:
Tarehe 14.8.2014
Naibu Waziri wa Habari, Utamadun,Vijanai na Michezo Mheshimiwa Amosi
Makala aliitisha kikao cha pamoja, kilichojumuisha pande zote husika
wakimwemo wasaidizi wake, shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi wa
Yanga sc na uongozi wa Azam Media.
Baada ya kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa
(a)Klabu
ya Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia katika utengenezaji wa
mkataba wa udhamini wa haki za matangazo na televisheni wa Azam Media
ili kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba kwa namna yoyote
haviathiri klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam Media
wanaotarajiwa kupewa haki hizo na Timu ya Mpira Azam FC moja ya timu
pinzani ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom
(b)Kuwepo
na utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na uongozi wa Yanga
kuzungumzia mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande zote mbili.
Hivyo
basi baada ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa taarifa kwa
wanachama wake kuwa mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti 2013,
viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa
hadi mtakapotangaziwa vinginevyo, lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa
uongozi kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo juu
Pia
uongozi unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga kwa kuonyesha
ukomavu na kusimamia maendeleo ya klabu yetu kwa Hali na mali, na
uongozi Utaendelea kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi
pia unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani kuishangilia timu
yetu wakati wa mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa
michuano ya kutetea ubingwa tunaoushikiria wa Ligi Kuu ya vodacom
Clement Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young Africans Sports Club
16.08.2013
Kwa niaba ya website ya yanga
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA