Mh Bimani: Kusini Unguja musikubali kutumiwa na CCM kupiga kura kumi bila ya kuwa na maslahi bora
Mh Bimani
Wajumbe
wa mkutano mkuu CUF wilaya ya kusini Unguja wametakiwa kujitaarisha
vyema kwa kugombe nafasi mbali mbali za uwongozi ndani ya chama hicho
katika uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwana huu.
Kauli hio imetolewa na mkurugenzi wa haki za Binadamu habari uenezi na
mawasiliano ya umma wa chama cha wananchi CUF Mh,Salim Bimani wakati
alipokuwa akifungua rasmi mkutano mkuu wa wilaya ya kusini Unguja
uliokuwa na lengo la kujadili mambo mbali mbali katika harakati za
kuendeleza chama hicho katika mkoa wa kusini Unguja.
Mkutano
huo umeshirikisha wajumbe hamsini kutoka majimbo mawili ya wilaya hio
ambayo ni Muyuni na Makunduchi na umefanyika Makunduchi.
Mh,Bimani wakati akifungua mkutano huo amesema kuwa chama cha wananchi
CUF ndio chama pekee katika nchi hii ambacho kila lengo na dhamira ya
kuhakikisha kinaivuusha Zanzibar na hatimae kuwa nchi yenye mamlaka
kamili na kisha kutambulika kitaifa na kimataifa.
Amewataka
wajumbe hao kuhakikisha wananfanya utafiti wa kina kabla ya chaguzi za
chama zinazokuja hivi karibu ili kuepuka kuingiziwa virusi ndani ya
chama jambo ambalo litaweza kutupotezea dhamira ya kuipata Zanzibar
yenye uhuru wake kamili.
‘’Kama munavojua ndugu wanachama nchi
yetu kwa sasa imekabiliwa na mambo muhimu sana miongoni mwa mwambo hayo
ni hili la kuipata Zanzibar yetu hivyo basi hatuna budi kuungana na
kushikamana vizuri juu ya hili na tusikubali katu mwengine
kutuharibia’’alisema Bimani.
Aidha aliwafahamisha wajumbe hao
kuwa chama cha wananchi CUF tokea zamani kilisimama na hoja ya serikali
tatu kwa ajili ya maslahi ya wazanzibar waliowengine na sio serikali
mbili kama ilivo hivi sasa ambavyo wenzetu wasioitakia mema Zanzibar kwa
ajili ya maslahi yao binafsi wanavotaka,hiyvo kutokana na haya kuna
kila haja ya wazanzibar wote kuzidi kukiunga mkono chama hicho kwa ajili
ya maslahi ya nchi yao.
Wakati akiendelea kuzungumza na
wajumbe hao aliwaasa kutokuchokozeka hususani katika kipindi hichi
kizito kwa nchi yetu badala yake wawachie tu CCM na wazimu wao’’umeona
wapi chama cha siasa takribani miaka hamsini sasa kinaongoza nchi bila
ya kuwa hata na maendeleo kilichobaki kwao nikutukana tu majukwani kama
sikuishiwa kisera unadhani ni nini pumbavu likipumbaa pumbaa nao
’’alieleza Bwana Bimani.
Alieza kwamba CUF ni chama kinachojua
siasa hivo basi kutokana na taratibu za kisiasa CUF Hawezi kukaa
hadharani na kujibu matusi kama wananvofanya CCM kwani huo ni ujinga wa
hali ya mwisho na ni wazi kuwa kufanya hivo ni kuishiwa sera na ndio
mwisho wa kifo chao.
Lakini pia aliwanasihi wajumbe wa mkutano
huo kutokuwa waoga kabisa na wafanye jitihada za kuwashawishi vijana
kugombe nafasi ndani ya chama hicho kwani vijana ndio tegemeo kubwa
katika mustakbali wa nchi hii.
Hakuna asiejua kuwa CCM
huwatumia vijana wa kusini katika kipindi cha uchaguzi ili wapige kura
zaidi ya kumi lakini nataka niwaambie kuwa kwa sasa majimbo mengine
wameamka na hawataki tena wasiohusika kupiga kura katika majimbo yao
hivyo vijana watakaokubali kutumiwa na kujaribu tu kupiga kura sehemu
zisizokuwa zao basi kitakachowafika shauri yao.
‘’Ni mara ngapi
vijana wenu wametumiwa kupiga kura zaidi ya moja na je nyinyi
mumefaidhika na maendeleo gani huku Makunduchi hadi leo hii,musikubali
washawishini vijana waamke huu sio muda tena wakukubali kutumiwa na CCM
wenye lengo la kuiweka nchi rehani eti kwa kwakuwa wanapewa alfu kumi
baada ya kupiga kura’’alisema Bwana Bimani.
Hata hivyo
aliowaomba wajumbe hao kutochoka kabisa na suala hili badala yake
wasimame kidete mpaka pale watakapohakikisha Zanzibar inashika mamlaka
yake na hatimae kupachika bendera yake umoja wa matafa.
Nae
katibu wa CUF wilaya ya kusini Unguja Bwana Mohammed Kombo alimshukuru
Bwana Bimani kwa kukubali kwake wito wa kuja kufungua mkutano mkuu huo
wa wilaya ya kusini Unguja kukubali kwake nikuonesha mshikamo imara
uliopo ndani ya chama hicho.
Lakini pia alimuhakikishia kuwa
wao kama viongozi wa wilaya hio watafanya kazi kwa jitihada zote ili
kuhakikisha kuwa wananchi wa kusini Unguja wanazidi kuamka na kuitakia
mema nchi hii.
Mkutano huu mkuu wa wilaya ni mikutano ya
kawaida ndani ya chama ambayo hufanyika katika wilaya zote za Unguja na
Pemba kwa lengo la kuimarisha chama