Oct 17, 2013

JAMANI NISAIDIENI,MWENZENU NATESEKA


 MTOTO SULEIMAN RAJAB AKIFANYA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA MUNIRA BLOG LEO HII,ALIPOTEMBEWA NA WANA MUNIRA NYUMBANI KWAKE KIVULE 


"Jamani nisaidieni nipate matibabu,bora nikatwe miguu,kuliko hali hii".

Hayo yamesemwa leo hii na mtoto Suleyman Rajab Yusuf Upinde (14) wakati alipotembelewa na baadhi ya viongozi,wazazi na wanafunzi wa Munira Madrasa ya magomeni makuti Jijini Dar es salaam.

Amesema tokea apate akili amejikuta akiwa katika hali hiyo,hali ambayo inamnyima raha.

Akiongea kwa masikitiko alisema kwamba "nasikia maumivu makali,miguu inawaka moto kiasi kwamba naona bora nikatwe miguu,najuwa nitauguza kidonda,lakini bora ya hivyo kuliko hali hii".

"Natamani kutoka nje nicheze na wenzangu,lakini siwezi,natamani nikasome madrasa kama wanavyosoma wenzangu lakini siwezi na hata nikiwa mkubwa sintoweza kuowa kwa kuwa hakuna atakaye kubali kuolewa na mimi"alisema kwa masikitiko.

"Pamoja na hayo naamini kwamba tatizo hili kanipa Mungu na yeye ndiye pekee mwenye uwezo wa kuniondolea,lakini kwa kweli nasikia uchungu mimi kuwa hivi natamani niwe kama wenzangu"kauli ambayo iliwaliza wana munira wote walikwenda hapo kwa dhamira ya kumfariji.
 
Awali bwana Rajab Yusuf Upinde ambaye ni baba  mzazi wa mtoto huyo akiongea na wana Munira hao alisema,mtoto wake alizaliwa akiwa na uvimbe kidogo chini ya nyayo,licha ya juhudi za kumpeleka Hospitali,lakini hakupata unafuu zaidi ya uvimbe kuzidi siku hadi siku.

"Mwanangu hakuwahi kusimama dede kutokana na tatizo hili,kiasi kwamba kipindi chote cha kukuwa kwake hajawahi kujimudu zaidi ya kuhudumiwa,leo ili nimtoe nje ni lazima nimuweke katika hili shuka,kisha mimi nishike upande huu na mke wangu ashike upande huo ndipo tumtowe,peke yako huwezi kumbeba,"alisema kwa huzuni.

"Ilifikia hatua madaktari wa Hospitali ya CCBRT walishauri akatwe mguu,mama yake (ambaye kwa sasa amefariki) alikataa,lakini kwa hali ilivyo hivi sasa mgonjwa mwenyewe yupo radhi akatwe mguu,alisema.

Kwa upande wake bi Khadija Hemed Mpoto ambaye ni mama mlezi wa mtoto huyo alisema tokea aishi na mtoto huyo,sasa ni mwezi wa tatu na anaona uvimbe unazidi siku hadi siku.

"Huyu ni mume wangu kanioa miaka mingi,lakini baada ya mama wa Suleiman kufariki nilimshauri mume wangu amchukue huyu mtoto (kutoka kwa bibi yake) ili tuishi naye"Alisema bi Khadija.

Aliendelea kusema kwamba hali ya uvimbe inazidi siku hadi siku,binafsi namuonea haruma sana,kwani marafiki wake wanakuja kucheza nae,lakini wakiondoka tu unamuona wazi anakuwa mnyonge.

Akijibu maswali ya kiufundi kutoka kwa mwandishi wa munira blog Bi Khadija alisema,"leo mumemkuta baba yake kwa kuwa ni sikukuu,lakini si mkaaji wa nyumbani kwa sababu ya kutafuta rizki".

"Mimi ndiye nimuangalie kwa usafi,yeye (Seleman) mwenyewe hajiwezi kwa lolote,akitaka kujisaidia haja kubwa na ndogo nimletee beseni,nimuandalie na kumletea chakula lakini pia hata nguo nimveshe,wallahi nayafanya haya kwa moyo mmoja"alisema.

"Mbali ya kuwa na nidhamu mwanana lakini huyu ni mtoto anayehitaji malezi na huruma zetu,sasa nawajibika kumpenda kama ninavyowapenda watoto wangu wanne".Mwisho wa kumnukuu.

Mwandishi wa habari pamoja na wana munira walijionea uduni wa maisha yanayowakabili sambamba na hali halisi ya mtoto huyo ambapo kipindi chote walichokuwa hapo walibubujikwa na machozi ya wazi wazi.

"Kwa kweli haya ni mazingatio makubwa sana ambapo tunapaswa kuwa nayo,huyo ni mtoto mdogo,tusiamini kwamba kamkosea ALLAH hii ikawa ndiyo adhabu yake,wala tusiamini uzima tulionao eti kuna zuri tumemfanyia ALLAAH,sasa ni vyema tukamshukuru mungu kwa vitendo juu ya neema ya ukamilifu wa viungo aliyo tujaalia"alisema Ustaadh Ally Salum Jongo ambaye ni Mwenyekiti wa Muniira Madrasa And Islamic Propagation Assosiation alipokuwa anatoa nasaha chache.

Taasisi ya Munira Madrasa ina utaratibu wa kuwatembelea wagonjwa kila inapofika Sikukuu ya Idd mosi ya Mfungo tatu.

Kwa mara hii iliamua kumtembelea mtoto huyo baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa mtoto huyo mwenye maradhi ya ajabu.

Mbali ya kumpa vyakula kwa ajili ya Sikukuu lakini pia ilimpatia pesa taslimu shilingi laki moja (100,000) kwa ajili ya matibabu.

Mtoto huyo yupo kijiji cha kivule eneo la bomba mbili,manispaa ya Ilala mkoa wa Dar es salaam.

Taasisi ya munira inatoa wito kwa taasisi,mashirika na hata watu binafsi kumfariji na kumsaidia kimatibabu mtoto huyo,kwani kwa hakika mtoto Suleiman  anateseka.

Namba ya simu ya baba yake ni 0718 35 55 63.

MTOTO SULEIMAN AKIWA KAUSIMAMISHA MGUU,LAKINI HAWEZI KUUNYOSHA,NA ILI AUSIMAMISHE KAMA UNAVYOUONA NI LAZIMA APATE MSAADA WA KUUINUWA MGUU WAKE. 
 
  KWA HAKIKA MUNGU NI MKUBWA NA NI MUWEZA WA KILA KITU. 



 KUSHOTO NI MWENYEKITI WA MUNIIRA MADRASA USTAADH ALLY JONGO,ANAYEFUATA NI RAJAB YUSUF (BABA MZAZI WA MGONJWA) ANAYEFUATA NI MTOTO SULEIMAN (MGONJWA) ANAYEFUATA NI BI KHADIJA (MAMA MLEZI WA MGONJWA) NA MWISHO NI KATIBU WA MUNIIRA MADRASA USTAADH JUMA RASHID AMBAYE PIA NI MKURUGENZI WA MUNIRA BLOG.



 WANA MUNIRA WAKITOKWA NA MACHOZI LEO HII BAADA YA KUSHINDWA KUJIZUWIA KUTOKA NA HALI TETE ALIYONAYO MTOTO SULEIMAN.
 
 BIBI AKIDA AMBAYE NI MMOJA WA WANA MUNIRA AKIMKABIDHI MTOTO SULEIMA PESA TASLIM SHILINGI LAKI MOJA KWA AJILI YA MATIBABU. 
  
 Mtoto Suleiman akiwa na ndugu zake,rafiki zake pamoja na Abdul Azizi kutoka Muniira Unity Brothers. 
 
MWENYEKITI NA KATIBU MKUU WA MUNIIRA MADRASA AND ISLAMIC PROPAGATION ASSOCIATION
WAKIMFARIJI MTOTO SULEIMAN MWENYE UGONJWA WA AJABU. 

 
MWANDISHI WA MUNIRA BLOG AKIMUHOJI MAMA MLEZI.  
 
  BI KHADIJA MAMA MLEZI WA SULEIMAN,AKIJIBU MASWALI YA MWANDISHI WA MUNIRA BLOG.  
  
 BWANA RAJAB YUSUF AMBAYE NI BABA MZAZI WA MTOTO SULEIMAN
  
  WANA MUNIRA MADRASA WAKIWASILI NYUMBANI KWA MGONJWA. 
chanzo cha habari hii na http://muniramadrasa.blogspot.com

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA