Oct 17, 2013

Wamiliki wa kontena lililokuwa limebeba vitu vya ajabu na kuingizwa kupitia Mombasa wajitokeza

Wamiliki wa kontena lililokuwa limebeba vitu vya ajabu na kuingizwa kupitia Mombasa wajitokeza
Wamiliki wa supermarket ya Village Market ya nchini Kenya wamejitokeza na kudai kuwa vitu vilivyokuwa kwenye kontena lilikamatwa Mombasa ni vya kwao.

Wamesema waliagiza vitu hivyo kutoka China kwaajili ya sikukuu ya Kimarekani ya Halloween baadaye mwezi huu.

Katika maelezo yake, wameandika:

Market Masters LTD, hereby confirms that indeed we have ordered for the Halloween decorative items imported from China in container number PCIU 8125750, and are not restricted items.

Just like during Easter Holiday or Christmas season, the items in question are solely used for decorating the entire shopping centre for our annual Halloween parties held within village market every last Saturday in October, for the past 17 years.

We needed to replace the old worn out ones with us, in readiness for our upcoming Haloween party slated for 26th October 2013.”

Kontena hilo lilikuwa na wanasesele wa kutisha, wanaonekana wakiwa na maumivu makali, mikono na miguu iliyokatwa, maiti na vitu vingine vilivyodaiwa kuwa vya kishetani.

Awali, vitu hivyo vilidaiwa kuwa vya mwanasiasa maarufu wa Kenya, aliyewahi kuwa naibu waziri wa zamani, Omingo Magara ambaye alilazimika kujitokeza na kukanusha japo alikiri kuwa baadhi ya vitu vyake (tofauti kabisa na vitu hivyo vya ajabu) vilikuwemo ndani ya kontena hilo.

Na sasa ameitaka mamlaka ya mapato nchini humo, KRA kumwomba radhi na kama ikishindwa ndani ya siku 7 ataipeleka mahakamani.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA