Jul 3, 2012

MISRI Yaahirisha Mechi Dhidi Ya Ngorongoro HEROES

Mechi mbili za kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na Misri zilizokuwa zichezwe mwezi huu zimefutwa.

Chama cha Mpira wa Miguu Misri (EFA) kimetuma taarifa jana (Julai 1 mwaka huu) kikiomba kusogezwa mbele hadi mwishoni mwa Agosti baada ya kushindwa kupata usafiri wa ndege kuwahi tarehe ambazo ilikubaliana na TFF kwa ajili ya mechi hizo.

Ngorongoro Heroes ambayo tayari iko kambini ilikuwa icheze mechi hizo Julai 3 na 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuikabili Nigeria katika mechi ya michuano ya Afrika, Julai 29 mwaka huu.

Mechi nyingine za kirafiki kwa Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Jakob Michelsen zitachezwa Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA