Haruna Niyonzima akiongea na waandishi wa habari baada ya kuongeza mkataba wa kuichezea Yanga kwa miaka miwili
Uongozi wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom klabu ya Young
Africans leo umekata mzizi wa fitina kwa kiungo mchezeshaji kutoka
nchini Rwanda Haruna Niyonzima kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa
mkataba wa miaka miwili kufuatia kumalizika kwa mkataba wake awali.
Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu
Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo
kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka
miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
Mwalusako
amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima,
baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu
yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na
ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna
Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea
katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili
aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya
ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye
Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu
ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani
najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili
iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti
wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema
palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu
Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"
Tunautambua
mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe
viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea
mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia
timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
1 Weka maoni yako hapa:
kweli yanga noma
Post a Comment
COMMENT HAPA