Zitto akihutubia maelfu ya wafuasi wake
Mh.Zitto Kabwe ameshawasili kwenye Viwanja hivi vya Mwanga CENTRE na
Utambulisho unaendelea kwa viongozi wa chama,Kubwa ZItto ni Mbunge wa
Kitaifa,Wanakigoma hawababaishwi na ubaguzi unaeondelea CHADEMA.
MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA KIGOMA
Wanakigoma,ZItto ni mmoja wa vijana wa kigoma,tunakila sababu ya
Kumlinda,kumpigania na kusimama naye katika hatua zozote zile.Naomba
tuungane kupambana naye kwenye hatua hii inayaoendelea ndani ya chama.
Inauma sana kuona tumepigwa mabomu,risasi,tumetumia muda wetu kuijenga
chadema,Leo matunda yameanza kutoka wanakata mti kwasababu tu wao
wanataka kujinufaisha.HAPANA.
KATIBU CHADEMA MKOA ANASEMA
Nimeulizwa mwasali mengi sana kwanini hakuna bandera,kwanza ni salamu
kwa Katibu Mkuu kuwa Chadema Kigoma hatuna bendera,fedha za kununulia
hatua(ruzuku).Pia mapokezi ya zitto licha ya kuwa ya chama,ZItto
tumempokea Kitaifa.
Zitto akiwasalimia maelefu ya Wanakigoma
Nimekuja kuzungumza nanyi wanakigoma kwa Mujibu wa katiba ya chama,kama
Katibu Mkoa alivyoeleza na katibu wa chadema hapa Kigoma mjini.
Hivyo msithubutu kusikia propaganda zozote zile eti nitawajibishwa
kwasababu ya kufanya mikutano nje ya Kigoma kaskazini,katiba ya chama
inaniruhusu na katiba ya nchi inaniruhusu pia kwenda popote na kufanya
chochote bila kuvunja sheria.
Wote mnakumbuka nilichukulia kadi kwenye uwanja huu mwaka 1993 nikiwa na
miaka 16. Nimepata Ubunge nikiwa na miaka 29 kwenda kuwawasilisha
wananchi wangu wa kigoma kaskazini na nchi nzima. Mnakubaliana nami
namna nilivyokuwa kiongozi bora ndani ya bunge,Kuanzia hoja ya
Buzwagi,Kumng'oa waziri mkuu na sasa Mabilioni ya Uswis.
Pia namna nilivyopigania ujenzi wa rami mkoa wa Kigoma,Lakini lengo
langu ni kutaka siku zote wanakigoma mjivunie kutaja kuwa ww ni mzawa wa
kigoma,na nimeshaijenga heshima hiyo.
Lakini ndugu zangu Ng'ombe akiumizwa malishoni anakimbilia zizini.
Nimekuja Nyumbani kuzungumza na wananchi wangu, Ndani ya chama
nimeumizwa ,Nimevumilia sana kwa mikuki ninayopigwa na wenzangu ndani ya
chama.
Uchaguzi wa ndani ya chama wa Uliopita nilijitosa kugombea
Uenyekiti,Lakini wazee wa chama wakaniita nimuachie mwenzangu awe
mwenyekiti, NIKAKUBALI.
Lakini kuna vijana wamesurubiwa ndani ya chama kwasababu tu wamekuwa
wakiniunga mkono. Mchange Habib alishinda uchaguzi wa Umoja wa Vijana,
Lakini matokeo yake yakafutwa na kupewa mtu mwingine, Kwasababu yangu.
Akina Kafulila pia walishughulikiwa ndani ya chama kwasababu ya Kudai
haki,Bahati mbaya sana Kafulila akaondoka kwa hasira chadema.
MIMI NITAPIGANIA HAKI YANGU kwa sababu ndani ya chadema kuna jasho
langu, Kuna nguvu na mali zangu nilizopigania, Kuna watanzania
waliopigwa risasi, mabomu na wengine kufariki kwasabau ya kupigania
chadema.
KUONDOKA CHADEMA NI KUWASALITI WAPIGANIA HAKI, KUWASALITI WALIOKUFA KWASABABU YA KUIPIGANIA CHADEMA ISIMAME HADI HAPA ILIPO.
Pia naomba mtambue hoja yangu ya PAC inanimaliza chadema,Wenzangu ndani
ya chama wananiandama kwasababu sikuwajulisha mapema kuhusu mahesabu ya
ruzuku/mapato ya chama. Hakika katika hili nitaendelea kusimamia hoja
yangu kwa Maslahi ya chama,Chadema lazima ikaguliwe kwa mujibu wa kanuni
na sheria za nchi.
Jana mmesikia Slaa kwenye vyombo vya habari akisema atanifukuza eti
vijana wanaoniunga mkono na wananchi wananiponza,Watanzania hukusio
kufukuzwa??
Slaa ni katibu Mkuu wa chama na ndiye mwendesha vikao,Leo hii anatoa huku kabla ya Vikao,huku sio kufukuzwa?
Mwenyekiti wa chama pia alinukuliwa na vyombo vya habari kule mwanza,Eti
zitto akirudishiwa vyeo vyake ndani ya chama labda mimi sio Mbowe!
Wanzania huko sijafukuzwa tayari?
Leo hii wajumbe wa mkutano mkuu wameshaanza kuandikisha majina yao
wakiomba mkutano mkuu uitishwe ilikujadili hatma ya mambo yanayoendelea
ndani ya chama,Pia kujadili rufaa yangu. LAKINI DR. SLAA ANAWATISHIA ETI
WAOAFANYA HIVYO NI WASALITI NA WAHUJUMU WA CHAMA!
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA