Rais wa Nigeria amelaani mashambulizi yaliyotokea mjini Jos ambapo takriban watu 200 na zaidi wameuawa leo Jumanne jioni.
Rais Jonathan amesema kuwa waliotekeleza mashambulizi hayo ni watu wenye unyama na wakatili.
Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Inahofiwa kuwa miili zaidi bado iko chini ya vifusi ya majengo yaliyoharibiwa na milipuko hiyo , ambayo ililenga soko lililokuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na hospitali
Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imetegwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Athari za mlipuko mjini Jos Nigeria
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na
shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa
kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameseama hatakomesha juhudi za kuangamiza kabisa ugaidi.
'Mji muhimu'
Mji wa Jos unatazamiwa kuwa mji mkuu wa jimbo la
Plateau ambalo liko katika eneo la katikati linalo tenganisha kaskazini
iliyo na raia wengi zaidi wa kiislamu, na kusini lililojaa wakristu
zaidi.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP 2012
ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi ya
New Bo...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA