Jun 15, 2012

Matukio mbalimbali Tuzo za TASWA.2011-2012

 
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Olimpiki Maalum Heri Suleiman

  
Mchezaji wa zamani wa timu ya Coast Union ya Tanga na Timu ya taifa Salim Amir akikabidhi tuzo kwa mchezaji Shomari Kapombe

  
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Agrey Morris katika hafla hiyo.

  
 Baba mwenye uzao wa mabondia Mzee Matumla kulia  akikabidhi tuzo ya mwanamchezo bora wa kigeni katika soka Emmanuel Okwi kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya mchezaji huyo, katika tuzo  zinazoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam

  
Mzee Ali Hassan Mwinyi akifurahia jambo wakati alipokuwa akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za TASWA Masoud Saanane katikati ni mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto

  
 Mwenyekiti wa TASWA akimkabidhi tuzo yake mchezaji bora wa  mchezo wa Netiboli Lilian Sylidion kutoka kutoka Shule ya Filbert Bayi.

  
 Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti  Bw. Richard Wells akijadili jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa KampunihiyoTeddy Mapunda  katika hafla hiyo

  
 Makamu Mwenyekiti wa Simba na Geofrey Nyange katikati akiwa katizo hafla hiyo kulia ni Jamal Rwambo mdau mkubwa wa michezo na kushoto ni Maulid Kitenge Makamu Mwenyekiti wa TASWA

  
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT Bw. Dioniz Malinzi, Mwenyekiti wa kampuni ya bia ya Serengeti, Mark Bomani, aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Richard Wells na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru


  Rais wa TFF, Leodegar Tenga wa pili kulia akiwa na Jellah Mtagwa kushoto kwake


Kaburu akimsaidia Kapombe kupokea tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka 2011 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA