Jun 14, 2012

Kuona Twiga Stars, Ethiopia 2,000/-

Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia itakayochezwa Jumamosi (Juni 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani na rangi ya chungwa. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 48,590 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi Grace Msiska atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Bernadettar Kwimbira, Happiness Mbandambanda na Linda Chikuni, wote kutoka Malawi. Kamishna ambaye anatoka Kenya ni Maqulate Atieno. Waamuzi hao wamewasili jana.
blog yenu ya Bongo Yetu inawahimiza wapenda soka wote kujitokeza kwa wingi kuisapoti na kuipa nguvu timu yetu ya taifa ya wanawake aka twiga stars

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA