Timu 10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya Rollingstone
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu itafanyika
Makamba nchini Burundi kuanzia Julai 7 mwaka huu.
Jumla ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa katika
makundi sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi, Kenya, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda na Zanzibar.
Timu za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam, Bishop
High School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting,
Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu zote
zinatakiwa kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili kuthibitisha
umri wao. Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu umri
wa mchezaji yeyote.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA