Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa
uchaguzi baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo
vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
FIFA ambayo ilituma
ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato
wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea
kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013,
lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji
wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
Raiswa TFF,
Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano
wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha
Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na
maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA,
Jerome Valcke.
Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga
safari kwenda Dodoma jana kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake
pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
“Matarajio
yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye
uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa
hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia
itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa
hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili
vya miaka minne kila kimoja.
“Lengo letu ni kuhakikisha maagizo hayo
yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe
iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili
tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na FIFA.”
Uchaguzi wa
TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa
ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua
ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika
barua FIFA kuomba iingilie kati.
Rais Tenga alisema kuwa ujumbe wa
FIFA ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na
kwamba baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa
yatakuwa ni suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa
mpira wa miguu nchini.
Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:
1.
Kuunda vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili
ambavyo ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake
yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;
2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;
3.
Kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua
milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura
kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati
hizo za maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu
wa Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.
Katika maoni yake FIFA
imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua au
kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya 9 (7)
ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo
vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za
shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata hivyo, FIFA
ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika
(kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.
“Kutokana
na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, m
moja wa wagombea amekuwa
akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni
ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.
Rais Tenga ameagiza
kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kupokea
maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa lengo la
kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA