Aug 22, 2012

YANGA YAELEKEA RWANDA


 kikosi cha timu ya Yanga 
Kikosi cha mabingwa wa vilabu Bingwa Afrika 

Mashariki na Kati (kombe la Kagame) timu ya Young Africans inaondoka mchana huu kuelekea nchini Rwanda kufuatia mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda


Akiongea na waandishi wa habari makao makuu  ya klabu, mwenyekiti wa timu ya Young Africans Yusuph Manji amesema wameitikia mwaliko huo wa rais mpenda michezo, hivyo wanaelekea Kigali wakiwa na furaha ya mwaliko huo, pia wakiwa kama mabingwa watetezi wa kombe hilo mara ya pili mfululizo linalofadhiliwa na Rais Kagame.

Aidha Manji amesema wanategemea kufungua tawi jipya la Yanga nchini Rwanda, hiyo itasaidia kuongeza wanachama nje ya nchi kwa kuanzia na Rwanda. 

Young Africans itakua nchini Rwanda kwa muda wa wiki moja ya mafunzo, ambapo inatazamiwa kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu za Rayon Sports, Police Force na timu moja ambayo watajulishwa na wenyeji wao chama cha soka nchini Rwanda.

Akiongelea suala la mchezaji mpya aliyesajiliwa kutokea APR ya Rwanda, Mbuyu Twite, Manji amesema mchezaji huyo wataungana nae nchini Rwanda na mara baada ya kambi hiyo ya wiki moja atarudi na timu kuja kuanza kuitumikia katika msimu mpya w aligi kuu.

Pia Manji amesema wanamshukuru Rais wa Jamuri ya muugano wa Tanzania mh.Jakaya Kikwete kwa kuwapa mwaliko wa kupeleka kombe hilo Ikulu, na kuahidi kwamba mara watakaporudi kutoka Rwanda wataitikia wito wake na kwenda kuonana nae.

Msafara unaondoka utakuwa na jumla ya watu 42, Wachezaji 29 na Benchi la Ufundi 5 na Viongozi 8
Viongozi wanaondoka ni mwenyekiti Yusuph Manji, makamu mwenyekiti Clement Sanga, Wajumbe wa bodi ya wadhamini Mama Karume, Francis Kifukwe na Seif Ahmed Magari.

Wajumbe kamati ya utendaji ni Abdallah Bin-Kleb, Salum Rupia.
Benchi la ufundi: kocha mkuu Tom Saintfiet, kocha msaidizi Fred Felix Minziro,, meneja wa timu Hafidh Saleh, daktari wa timu Dr.Suphian Juma na mtunza vifaa Mahmoud Omary (mpogolo)

Wachezaji wanaondoka ni:

Walinda mlango: Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez, na Said Mohamed

Walinzi wa pembeni: Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, Stephano Mwasika, David Luhende 

Walinzi wa kati: Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Ibrahim Job, Ladisalus Mbogo,

Viungo wa ulinzi: Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif 'Kijiko' Salum Telela

Viungo wa pembeni: Saimon Msuva, Shamte Ally, Omega Seme, Idrisa Rashid, Nizar Khalfan

Viungo washambuliaji: Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari

Washambuliaji: Said Bahanunzi, Hamis Kiiza, Jeryson Tegete na Didier Kavumabagu


Mwenyekiti wa Young Africans Yusuph Manji (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu, kulia kwake ni katibu mkuu Mwesigwa Selestine na kushoto kwake ni makamu mwenyekiti Clement Sanga
0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA