Droo ya makundi kwa ajli ya mashindano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati al-maarufu kama (KAGAME CUP) imefanyika leo mchana mjini Khartoum nchini Sudan huku Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Young Africans wakipangwa kundi C kwenye michuano hiyo itakayoanza 18 Juni - 2 Julai 2013.
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye imeonyesha mashindano ya mwaka huu itakua na jumla ya timu 13 kutoka katika nchi 10 wanachama ambapo droo hiyo imegawanyika katika makundi 3 ya A,B,C.
Timu zitakazo shiriki mashindano hayo na nchi zinazotokea kwenye mabano ni : Al-Hillal, El-Merreikh na Al Shandy (Sudan), Al Nasri (Sudan Kusini), Yanga & Simba (Tanzania), Express (Uganda), Tusker (Kenya), APR (Rwanda), Vitaloo (Burundi), Ports (Djbouti), Elman (Somalia) na Falcon (Zanzibar)
Aidha mashindano ya mwaka huu yameongeza zawadi kwa washindi kutoka kitita cha dola za kimarekani 60,000 mpaka kufikia dolla 80,000 ikiwa kuna ongezeko la dola 20,000 ambapo zawadi kwa washindi zitapangwa na kamati ya utendaji kabla ya mashindano kuanza.
Mashindano ya CECAFA mwaka huu yatafanyika nchini Sudan katika miji ya El-Fashir na Kadugli ambayo ni miji iliyopo kusini mwa nchi ya Sudan yenye wakazi wapatao milioni 34 na eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 1,886,068.
Makundi ya michuano hiyo itakayoanza mwezi ujao ni kama ifuatavyo:
KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER
KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar), Al Shandy (Sudan) - KADUGLI
KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR
KAGAME CUP FIXTURE 18th JUNE - 2nd JULY 2013 (EL-FASHIR & KADUGLI - SUDAN)
DATE | TEAM | TEAM | GROUP/TIME | VENUE |
18.06.2013. | TUSKER | SUPER FALCON | B - 2:00 PM | KADUGLI |
AL HILLAL | AL NASRI | B - 4:00 PM | KADUGLI | |
19.06.2013. | VITALOO | PORTS | C - 4:00 PM | EL-FASHER |
20.06.2013. | YANGA SC | EXPRESS | C - 2:00 PM | EL-FASHER |
20.06.2013. | ELMAN FC | APR FC | A - 4:00 PM | EL-FASHER |
20.06.2013. | SUPER FALCON | AL NASRI | B -2:00 PM | KADUGLI |
20.06.2013. | TUSKER | AL-SHANDY | B - 4:00 PM | KADUGLI |
21.06.2013. | EL MERREIKH | SIMBA SC | A - 4:00 PM | KADUGLI |
22.06.2013. | EXPRESS FC | VITALOO | C - 2:00 PM | EL-FASHER |
PORTS | YANGA SC | C - 4:00 PM | EL FASHER | |
22.06.2013. | AL NASRI | TUSKER | B - 2:00 PM | KADUGLI |
AL SHANDY | AL HILAL | B - 4:00 PM | KADUGLI | |
23.06.2013 | APR | SIMBA SC | A - 2:00 PM | EL-FASHER |
EL MERREIKH | ELAM FC | A - 4:00 PM | EL-FASHER |
24.06.2013 | AL NASRI | AL SHANDY | B - 2:00 PM | KADUGLI |
SUPER FALCON | AL HILLAL | B - 4:00 PM | KADUGLI | |
24.06.2013. | PORTS | EXPRESS FC | C - 4:00 PM | EL-FASHER |
25.06.2013. | VITALOO | YANGA SC | C - 4:00 PM | EL-FASHER |
26.06.2013. | AL SHANDY | SUPER FALCON | B - 2:00 PM | KADUGLI |
AL HILLAL | TUSKER | B - 4:00 PM | KADUGLI | |
26.06.2012. | SIMBA SC | ELMAN FC | A - 2:00 PM | EL-FASHER |
APR FC | EL MERREIK | A - 4:00 PM | EL-FASHER | |
27.06.2013. | REST DAY | REST DAY | REST DAY | REST DAY |
28.06.2013. | (23) B2 VS C2 | (24) B1 VS BEST Q | TBD | KADUGLI |
28.06.2013. | (25) C1 VS A2 | (26) A1 VS B3 | TBD | EL-FASHER |
30.06.2013. | WNR 23 VS WNR 25 | WIN 24 VS WIN 26 | TBD | |
01.07.2013. | REST DAY | REST DAY | REST DAY | REST DAY |
02.07.2013. | LOOSER | LOOSER 28 | 3RD - TBD | EL-FASHER |
WINNER 27 | WINNER 28 | FAINAL - TBD | EL-FASHER |
HABARI KWA NIABA YA http://www.youngafricans.co.tz