Ofisi za UN zashambuliwa Somalia
Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia makao ya umoja wa mataifa mjini Mogadishu Somalia .
Duru zinasema kuwa mshambuliaji wa
kujitoa mhanga ndiye alijilipua katika lango kuu la makao hayo kisha
watu waliokuwa wamejihami wakaingia ndani ya ofisi na kuanza kufyatua
risasi.
Makao yenyewe yako karibu na uwanja wa ndege na yana nyumba za wafanyakazi wa umoja wa mataifa .
Wavamizi walishambulia ofisi za makao ya shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
Majeshi ya Somalia na yale ya Muungano wa
Afrika, walizingira makao ya shirika hilo na kuanza kufyatua risasi
kujaribu kuwatimua washambuliaji hao.
Kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Ofisi
hizo ni makao kwa maafisa wa Umoja wa mataifa walio mjini Mogadishu.Hili
ndilo shambulizi kubwa zaidi kushuhudiwa kwa siku za karibuni dhidi ya
Umoja wa mataifa mjini Mogadishu
chanzo na http://www.bbc.co.uk
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA