CUF KULISHITAKI JESHI LA WANANCHI JWTZ
CHAMA
cha Wananchi (CUF) kinaandaa utaratibu wa kufungua kesi mahakamani
dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Wanajeshi wa Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa watendaji wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi
Mipango, Uchaguzi wa Bunge Shaweji Mketo,kwa niaba ya wanachama wenzake
alisema, bado wanawasiliana na wanasheria, taasisi za haki za binadamu
na mamlaka nyingine ili kupata mwongozo waweze kufungua kesi hiyo.
Mketo na wenzake watano, ni miongoni mwa watu walioonja joto ya mateso
ya siku 28 kutoka kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambao
wameweka kambi Mtwara kudhibiti machafuko yanayotokana na madai ya
kuzuia bomba la gesi asilia lisijengwe Dar es Salaam.
Mbali na Mketo wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Mtwara mjini Salum
Mohamed, Mwenyekiti wa Mtwara mjini Salum Mohamed, Mwenyekiti wa Wilaya
Mtwara vijijini Ismail Jamal,Katibu wa Wilaya Mtwara mjini Said Kulaga
na dereva wa CUF makao makuu Kashinde Juma.
Akisimulia mkasa
huo uliompata yeye na wenzake alisema wakiwa njiani walikutana na gari
mbili za jeshi kubwa na ndogo zikiwa njia panda ya newala na mtwara
mjini,na kuwasimamisha huku walitokea askari wapatao 50 vichakani na
kuanza kuwapiga huku wakiwasachi mifukoni.
“Askari wa JWTZ
walikuwa 50 walitusachi na kuchukua fedha zangu shilingi 85,000 na
nilipoanza kuzuia fedha hizo wasizichukue ndipo walipoanza kunipiga
kweli wakanivua viatu vyangu nilivyowahi kununua nje ya nchi
wakavichukua na mimi kuniachia vyao vya jeshi hivi hapa ,”alieleza
Mketo.
Alisema walikuwa wakipigwa na fimbo, kumwagiwa maji
yaliyokuwa yamewekwa barafu na pilipili jambo ambalo liliwafanya
waendelee kupata maumivu makali sana.
Mketo alisema hata hivyo
kuteswa kwao ni ishara kuwa Mtwara bado inanuka damu na hakuna usalama
huku wananchi wengi wakihofiwa kufariki dunia.
Hata hivyo
alisema wakati wakiendelea kuwatesa alisikika mwanajeshi mmoja akisema
wao wapo pale kwa ajili ya kutekeleza amri ya Waziri Mkuu aliyoitoa
Bungeni kwamba wananchi watakaokaidi amri ya serikali wanatakiwa
kupigwa.
Kiongozi huyo ambaye aliongea kwa masikitiko makubwa
huku akiwataka wenzake kuonesha majereha kwa wanahabari alisema kuwa
licha ya kuwaambia wanajeshi waliokuwa wakiwatesa kuwa amefanyiwa
upasuaji mkubwa wasimpige eneo hilo hawakujali kwani waliendelea
kumchapa na bakora katika eneo la mshono hadi lilipogeuka rangi na kuwa
nyeusi.
Alisema kiongozi mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Mtwara
mjini Salum Mohamed aliambiwa azivute ndevu zake kwa kutumia mikono na
alifanya hivyo hadi haapo zilipoanza kuvuja damu ndipo wakamwambia
walichokuwa wanakihitaji.
Mketo alisema vitendo hivyo ni vya
kinyama na kwamba haviwezi kuvumilika hivyo serikali inatakiwa
kuviangalia utendaji kazi wa vyombo vya dola kwani ni kulinda raia na si
kutesa.
Hata hivyo aliilaumu serikali kwa kuvifungia vyombo
vya habari mkoani humo kwa kigezo cha kwamba vinawashawishi wananchi
kuandamana jambo ambalo si kweli.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA