Jul 25, 2013

JAVU AANZA KAZI YANGA

     Mshambuliaji mpya wa timu ya Yanga Hussein Javu               

Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji Hussein Javu kutoka timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani - Morogoro ambapo mchezaji huyo leo ameanza mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola Mabibo jijini Dar es salaam.

Usajili wa Javu unafikisha idadi ya washambuliaji sita mpaka sasa wakiwemo Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Said Bahanuzi, Shaban Kondo (mpya - Msumbiji) na Realintus Lusajo (mpya kutoka Machava FC - Moshi).

Kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kinaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza agosti 24 kwa kufungua dimba na timu ya Ashanti United iliyopanda msimu huu.

Agosti 17-2013  Young Africans itacheza mchezo wa Ngao ya Hisani na timu ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu kwa msimu wa 2013/2014.

Mpaka sasa klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji saba (7) wapya ambao ni:

1. Deogratius Munishi 'Dida' -  Huru Azam FC (Golikipa)
2.Rajab Zahir -  Huru Mtibwa Sugar  (Mlinzi wa kati)
3.Hamis Thabit - Huru Ureno (Kiungo)
4.Shaban Kondo - Huru Msumbuji (Mshambuliaji)
5.Mrisho Ngassa - Huru Azam FC (Kiungo mshambuliaji)
6.Reanlintus Lusajo - Huru Machava FC (mshambuliaji)
7. Hussein Javu - Mtibwa Sugar (mshambuliaji)

Kikosi kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kila siku saa 2 asubuhi na wachezaji waliopo katika timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) wanatarajiwa kuungana na wenzao katika mazoezi siku ya jumatatu.

chanzo na http://www.youngafricans.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA