Aug 26, 2013

Hofu imewapata waumini wa KKKT kijitonyama baada ya kinachosadikiwa kuwa bomu kurushwa hapo.

 

Hali ya taharuki imezuka katika eneo la kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania usharika wa kijitonyama na maeneo ya jirani yake baada ya kugundulika kuwepo kwa kitu kilichohisiwa kuwa ni bomu kikiwa karibu na transfoma iliyopo ndani ya uzio wa kanisa hilo. 


Kitu hicho ambacho kilifungwa katika boksi ambalo liliwekwa juu a transfoma na kisha kufungwa na kamba umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo kilisababisha taharuki kanisa hapo na shughuli mbalimbali za ibada zilizokuwa zikiendelea kusitishwa ghafla.

Mchungaji kiongozi wa usharika huo wa kijitonyama  Ernest Kadiva amesema walipigwa na mshangao baada ya kuona uwepo wa kitu hicho hali iliyowafanya kuwapigia simu viongozi wa polisi ili waende kubaini kama ni bomu au la.

Naye mkuu wa upelelezi katika kanda maalum ya Dar es Salaam Hemed Msangi ambaye alifika eneo hilo dakika chache baada ya kugundulika kuwepo kwa kitu hicho amesema uchunguzi wa awali umebaini kitu hicho siyo .

 Hata hivyo maelezo hayo ya mkuu huyo wa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam hayakukata kiu ya itv kujua kama ni bomu au la hali iliyomfanya kamanda Msangi pamoja na maafisa wa usalama wa taifa katika mkoa wa Dar es Salaam kufanya kikao cha dharura ikiwemo kuperuzi katika mitandao na kubaini kuwa kitu hicho huwa kinatumika katika masuala ya hali ya hewa hasa kwenye viwanja vya ndege.

 chanzo na http://www.itv.co.tz