Aug 26, 2013

Serikali imefunga mashine mpya zinazoweza kubaini madawa ya kulevya.



Serikali imefunga mashine mpya zinazoweza kubaini madawa ya kulevya.
  Serikali imefunga mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa kubaini aina yoyote ya dawa za kulevya na nyara za serikali kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-salaam, lengo likiwa ni kudhibiti uingizwaji na upitishwaji wa mizigo uwanjani hapo,ambapo kuanzia sasa mizigo yote inayoingia na kutoka itakaguliwa.

Waziri wa uchukuzi Mheshimiwa Dk Harison Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar-es-Salaam,mara baada ya kutembelea uwanja huo kwa mara ya pili ili kuona zoezi la ufungwaji wa mashine za kisasa zenye uwezo kutambua dawa za kulevya na nyala nyingine za serikali.

Meneja wa usala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Bwana Clence Jingu,amesema kuwa kufungwa kwa mashine hiyo ambayo itakuwa ikijiongoza yenyewe kwa kukagua mizigo ya abiria wanaoingia na wanaosafiri tofauti za zamani ambapo mizigo iliyokuwa ikiingia ilikuwa haikaguliwi.

Awali akiwa uwanjani hapo waziri Mwakyembe amewaagiza wasimamizi wa uwanja huo,kuhakikisha kuwa ombaomba wote wanaozagaa uwanjani hapo wanaondolewa mara moja,kwani uwanja huo ndiyo kioo na sura ya Tanzania ambapo ITV ilishuhudia baadhi ya abiria wakipita na kuwapatia ombaomba hao kitu chochote.

Katika tukio lingine waziri Mwakyembe alizuru ghafla kwenye mizani iliyopo maili moja kibaha mkoani Pwani, mara baada ya kupigiwa simu na mawaziri wa ulinzi na wa uchukuzi wa Zambia,wakidai kuwa raia wao wamezuiliwa kuondoka kwa mabasi yao manne yaliyopitia bandari ya Dar-es-Salaam kwa madai kuwa yamezidi viwango vya urefu kwa barabara za Tanzania ambapo walitakiwa kulipa faini ya dola za marekani ishirini elfu kwa kila basi moja.

 
chanzo na itv