Aug 19, 2013

KIIZA KWENDA LEBANON KWA MAJARIBIO




















 Hamis Kiiza 'Diego' akishangilia moja ya mabao yake aliyoyafunga dhidi ya Azama FC msimu uliopita
 
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda anayechezea klabu ya Young Africans Hamis Friday Kiiza 'Diego' kesho jioni anatarajia kusafiri kuelekea nchini Lebano kufanya majaribio ya wiki moja katika klabu ya Al Ahed SC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.
 
Kiiza ambaye mpaka sasa ameshaitumikia Young Africans kwa miaka miwili, aliongeza mkataba wa miaka miwili tena kuitumika klabu yenye maskani yake twiga/jangwani kufuatia kumalizika kwa mkataba wa awali ambapo sasa mkataba wake utamalizika mwaka 2015.

Al Ahed SC  Mabingwa mara tatu (3) wa kombe la Ligi Kuu nchini Lebanon, washindi mara nne (4) wa kombe la FA na washiriki wa kombe la Vilabu Bingwa barani Asia mara sita (6) wamekamilisha taratibu zote kwa ajili ya mchezaji kwenda kufanya majaribio.

Hamis Kiiza ataondoka kesho jioni kwa shirika la Ndege la Ethiopia ambapo ataanza mazoezi kwa siku saba (7) kuanzia alhamisi tarehe 22.08.2013 na anatajiwa kurejea nchini mwisho wa mwezi Agosti 31, 2013.

Wakati huo huo kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013 na mabingwa wa Ngao ya Hisani 2013/2014 leo wameendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa VPL dhidi ya Ashanti United siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jini Dar es salaam.

Katika mchezo dhidi ya Azam kugombea Ngao ya Jamii wachezaji Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na Ally Mustapha 'Barthez; walipata majeraha kufuatia kuumizwa na washambuliaji wa Azam John Bocco, Gaudence Mwaikimba na Kipre Tchetche hali zao zinaendelea vizuri.

"Leo wamefanya mazoezi mepesi isipokuwa Kelvin Yondani aliyepewa mapumziko na daktari kwa siku tatu (3) kufuatia kupatiwa matibabu ya nyama ya paja aliyoumia siku ya mchezo huo na anatajiwa kurejea dimbani siku ya jumatano kuungana na wachezaji wenzake katika mazoezi" alisema Dr Matuzya.

Young Africans inajiandaa na mchezo dhidi ya Ashanti United siku ya jumamosi tarehe 24.08.2013 utakaofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014.
CHANZO NA http://www.youngafricans.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA