Aug 16, 2013

Kikosi cha Coastal Union kuweka kambi mjini Moshi.

Kikosi cha Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kitaondoka jijini Tanga kuelekea mji msafi kuliko yote Tanzania, Moshi kwa ajili ya kuweka kambi ya siku kadhaa kabla ya kukutana na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao jijini Arusha.
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi Nassor Ahmed Binslum, timu imeamua kuelekea Moshi kutokana na hali ya hewa ya Mji huo kufanana na ya Arusha hivyo itasaidia wachezaji kuzoea hali ya baridi.
 
Kitu kingine alichozungumza Binslum ambapo walishauriana na kocha mkuu wa Wagosi, Hemed Morocco ni kuwafanya wachezaji kutoka nje ya mkoa wa Tanga kwani tangu walipoanza kukaa kambini hawajawahi kucheza nje ya mkoa huo mbali ya kufanya vizuri kwenye mechi zote za majaribio kitaifa na kimataifa.
 
Kwa maelezo ya kocha inabidi wachezaji wakae mbali na mashabiki ili kuona uwezo wao pindi wakicheza mechi za ugenini hasa ikizingatiwa ligi kuu itazitaka timu kucheza nyumbani na ugenini. 
 
Pindi watakapocheza nyumbani watapata mashabiki wengi lakini wakiwa nje ya Tanga watakutana na kelele za mashabiki wa timu pinzani zitakazowachanganya.
 
Mpaka sasa timu imepangiwa kuondoka Jumatatu ambapo jumamosi itaelekea Mombasa kucheza mechi moja ya kirafiki na kuelekea Moshi moja kwa moja.
 
“Timu itaelekea Mombasa jumamosi hii kucheza mechi moja ya kirafiki, halafu itaelekea Moshi itakapoweka kambi mpaka tarehe 24 mwezi huu watakapoingia Arisha kucheza na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi,” alisema Binslum.
 
Kutokana na usajili wa mwaka huu wapenzi wengi wa soka Tanzania wamekuwa wakiitabiria kufanya vizuri Coastal Union kwani  timu nyingi zimeshindwa kutumia vema nafasi ya kusajili wacezaji wenye uwezo. 
 
Coastal Union imefanikiwa kunasa wachezaji wawilai kutoka Simba SC, wawili kutoka JKT Oljoro, mmoja ktoka Jamhuri ya Pemba, mmoja kutoka Polisi Morogoro, mmoja kutok URA ya Uganda na mmoja kutoka Bandari ya Mombasa wakati mwingine ametoka Azam FC.
 
Mungu ibariki Tanga, Mungu ibariki Coastal Union.

COSTAL UNION
16 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
chanzo na  http://coastalunionsc.blogspot.com

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA