Sep 27, 2013

HUU HAPA UDHIBITISHO KUWA NGASSA KAMALIZANA NA TFF KESHO KUCHEZA MECHI

 
 Mrisho Ngassa (katikati) akionyesha risti ya malipo aliyopewa TFF baada ya kulipa deni la mil 45, kushoto kwake ni mhasibu wa Yanga, Rose Msamila na kulia ni Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia timu yake kuanzia kesho.

Ngassa ambaye aliambatana na viongozi wa klabu ya Yanga mjumbe wa sekretariat Partick Naggi, Afisa Habari Baraka Kizuguto na mhasibu Rose Msamila alikabidhi hundi za malipo kwa idara ya fedha ya shirikisho hilo.

Mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Ngassa aliongea na waandishi wa habari nje ya ofisi za TFF na kusema ameamua kulilipa deni hilo ili aweze kuitumikia klabu yake, kwani kukosa michezo sita kumemnyima fursa ya kuisaidia timu yake.

Naomba mnielewe hizi fedha nimezitoa mimi mwenyewe kwenye akiba yangu iliyopo bank, hivyo kama kuna mtu yoyote ataguswa na hili suala anaweza kuwasiliana na mimi katika kujaribu kunichangia juu ya hili.

Aidha Ngasaa amesema kwa sasa akili yake yote ipo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom na lengo lake ni kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya vizuri n akupata ushindi katika kila mchezo watakaocheza.
Kocha Ernie Brandts kwa sasa ana fursa ya kumtumia mchezaji Mrisho Ngasa kwa kuanzia kwa mchezo wa kesho kutokana na kuwa amekamilisha kila kitu.

Naye Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto amewaomba wapenzi, washabiki na wanachama kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Taifa kuja kuishangilia timu yao itakapokua ikicheza na maafande wa Ruvu Shooting.

Young Africans itacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
kwa niaba ya http://www.youngafricans.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA