Oct 29, 2013

Gari la Madam Rita, Mercedes Benz lateketea kwa moto likiwa barabarani

Gari la Madam Rita, Mercedes Benz lateketea kwa moto likiwa barabarani
Gari aina ya Mercedes Benz la Rita Paulsen aka Madam Rita limeteketea kwa moto likiwa barabarani Jumamosi iliyopita, Oct 26.

Hata hivyo kwenye gari hilo lililozimika barabarani na kuanza kuwaka moto, hakuwemo Madam Rita bali dereva wake, Julius Kanwakaita.

Chanzo kilichopelekea gari hilo kuwaka moto hakijafahamika mara moja.
August 21 mwaka jana, ofisi za kampuni yake ya Benchmark Productions zilizopo Mbezi Beach ziliteketea pia kwa moto  

chanzo na timesfm.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA