Oct 4, 2013

KUFUATIA KUUAWA MRITHI WA SHEIKH ABOUD ROGO, WAANDAMANAJI WACHOMA KANISA, MMOJA AJERUHIWA


Waandamanaji vijana wa kislamu wamejitokeza kupinga kile kinachodaiwa kuuawa kwa sheikh Ibrahim Ismail kwa kuchoma moto kanisa la Salvation Army huko mjini Mombasa.
 
Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi na risasi za moto kutawanya waandamanaji hao wenye hasira ambao walifunga barabara kwa muda kadhaa kwa kuchoma matairi ya gari.
Mitaa na maduka kadhaa yalifungwa katika kitongoji cha saba saba kufuatia ghasia hizo. Mashahidi walisema mtu mmoja alipigwa risasi na kujeruhiwa huko wilaya ya Majengo Mombasa. "Yeye alipigwa risasi tumboni na amechukuliwa kupelekwa Hospitali. Damu nyingi sana zimetoka ni kumuombea Mungu apone", alisema Salim Abdallah
Haikuwekwa wazi ni nani aliyempiga risasi.

Maandamano hayo yamesababishwa na watu wasiojulikana kuua watu wanne akiwemo Mhubiri maarufu wa kiislamu Sheikh Ibrahim Ismail jana usiku.


Sheikh Ibrahim alikuwa akipingwa na vyombo vya usalama vya nchini Kenya kwa kudaiwa kuchochea vijana kufanya vurugu na kuweka wazi msimamo wake wa kuunga Mkono Kundi la Al-Shabab 
 
  
polisi wakihaha kutuliza ghasia
  
Kanisa lililochomwa moto

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA