Kingwendu asimulia sakata la utapeli, 'nilimdanganya Bond mama anaumwa ili nikapige dili Msumbiji', ameyamaliza na amesaini kuwa chini ya Steps Entertainment
Kingwendu Ngwendulile, kama anavyojiita kiutani, amefunguka kiundani
kuhusu tuhuma zilizotolewa na muongozaji wa filamu wa kampuni ya Steps
Entertainment, Bond.
Akizungumza na Maryam Kitosi katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5
Times Fm, Mchekeshaji huyo amesimulia ‘picha’ ilivyokuwa hadi kufikia
hatua ya kudhaniwa kuwa amefanya utapeli, na kwamba yeye hakuwa na lengo
la kutapeli.
“Kiukweli ni kwamba, niseme tu labda kuna tamaa flani imenichukua.
Kwa sababu mimi niliingia mkataba na Mr. Bond kwamba bwana tutengeneze
filamu. Akaniuliza una kazi? Nikamwabia wiki hii niko free kama kawaida,
akasema okay tutaianza filamu yetu jumamosi tarehe 16. Baadae
akanipigia simu akaniambia, mtani wangu Kingwendu hii filamu tutacheza
tarehe 19 siku ya jumanne kwa sababu namalizia kupiga rangi ile nyumba.”
Amesimulia Kingwendu.
“Hapo hapo ananipa taarifa hiyo hapo na ikaja bonge la deal kutoka
Mozambique kutoka serikali ya FRELIMO, unaona bwana bonge la issue ya go
and return. Hebu niambie hata wewe, kwamba filamu inachezwa siku ya
Jumanne tarehe 19, mimi nahitajika kwenda kupiga kampeni Jumapili,
halafu Jumatatu narudi Dar es Salaam. Si naiwahi hiyo filamu ya bwana
Bond?”
Kwa kutompa presha mtayarishaji wa filamu hiyo, Kingwendu aliamua
kutumia ulimi wake vizuri, lakini bahati mbaya hakujua yatakayojili huko
Msumbiji.
“Bondi ningemwambia kwamba mimi naenda zangu Mozambique angemaindi,
kwa sababu tayari ameshaandaa kila kitu. Kweli huku na huku jinsi ya
kufanya, nikamdanganya Bond mimi naenda kwa mama kwa sababu mama
anaumwa, na kweli mama alikuwa anaumwa lakini bahati nzuri nilimtumia
fedha (kwenye ile advance aliyopewa ya laki mbili), nikampa mama laki
moja.” Kingwendu ameelezea mkasa huo.
“Kwenda kule, kumbe ile tiketi mimi sikuiangalia, kumbe ilikuwa
tiketi ya kwenda tu. Sio go and return! Sasa siku ya Jumatatu
nikaangalia tiketi naona tiketi sio ya go and return. Nikawaambia
waheshimiwa mbona hii tiketi sio go and return na mimi nina kazi ya watu
huko? Wakaniambia usiwe na wasiwasi, akatumwa mtu kwenda kukata tiketi
ya Jumatatu, akarudi anasema ndege imejaa ipo ndege ya Jumatano.”
Kingwendu ameeleza kuwa alipoona mambo hayaendi na anahitajika
Jumanne Tanzania, akatafuta line ya simu ya Msumbiji akampigia Bond
lakini hakupokea , na hata aliporudi akamtafuta akawa hapokei simu na
hata alipomtafuta hakuweza kumpata kiurahisi.
Hata hivyo, Kingwendu amedai kuwa alimpata Bond na uongozi wa Steps
Entertainment wakakaa wakayamaliza. Na habari njema ni kwamba walimsaini
moja kwa moja kuwa msanii wa kampuni hiyo.
Kwa hiyo Kingwendu yuko chini ya Steps Entertainment
chanzo na http://www.timesfm.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA