Dec 19, 2013

NDANI YA DAKIKA 90 YANGA KUVUNA MIL 90 CAF


  Katibu Mkuu wa Yanga Bw. Beno Njovu (kulia) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga. Kushoto ni mwakilishi wa kampuni ya SGM Bw. Francis Goitha

Klabu ya Young Africans SC imeingia mkataba wa kurusha mchezo wake wa hatua ya kwanza ya mashindano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Alh Ahly ya Misri kwa gharama ya dola za kimarekani elfu 55,000 sawa na mil 90/= za kitanzania kwa muda wa dakika 90.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Young Africans Katibu Mkuu  Bw. Beno Njovu amesema wameingia mkataba huo na kampuni ya SGM kutoka nchini Ufarans na moja kwa moja wameipa uwakala kampuni ya MGB ya Zamaleki ya Cairo.

Mkataba huo unawapa kibali kampuni ya SGM kurusha moja moja mchezo mchezo wa Yanga dhidi ya Al Ahly utakaofanyika Tanzania nchini Misri, nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Mbali huku pia vituo vya telesion vya ndani ya nchi vikipewa fursa ya kuonyesha ndani ya nchi.

SGM imefikia hatua hiyo kufuatia kuona ratiba ya Klabu Bingwa Afrika iliyotoka mwanzoni mwa wiki kuonyesha kuwa timu ya Young Africans itaanza na timu ya Komoronize katika hatua ya awali na kisha kukutana na Al Ahly katika hatua ya 32 bora.

Mwakilishi wa SGM Bw. Francis Gaitho amesema wao wameamua kuingia makubaliano hayo na Yanga mapema wakiwa na uhakika kuwa timu ya Yanga itasonga mbele katika hatua ya awali na hivyo watakutana na mabingwa watetezi Al Ahly.

Yanga itaanza kucheza na timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro Februari 8 mwakani uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana nao wiki baadae nchini kwao Comoro na kikifanikiwa kuvuka hatua hiyo ndo itakutana na Al Ahly Februari 28, 02, 02 Machi na kurudiana baada ya wiki moja nchini Misri.
   

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA