Dec 16, 2013

OKWI ATUA YANGA

  Emmanuel Okwi akiweka alama ya Dole Gumba mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Mashindao Musa Katabaro (kushoto) wakati akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016. kulia ni mwanasheria/meneja wa Okwi Bw. Edgar Agaba


Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.
 
Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.
 
Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku wa Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria  klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.
 
Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji  watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.
 
Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.
 
Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.
 
Baraka Kizuguto
 
 Afisa Habari – Young Africans SC
 
Disemba 15, 2013. 
  

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA