UNAJUA NI KWANINI WANAWAKE WENGI WAZURI HAWAOLEWI?
WATANZANIA wengi wanaamini, kwamba wanawake wazuri sana huwa hawaolewi. Kuamini huku bila shaka hakutokani na
utafiti wowote uwe rasmi au sio rasmi. Lakini wengi wanaamini hivyo.
Je, imani hii ina ukweli kwa kiasi gani? Swali hili bila shaka ni gumu kujibika. Labda tu kwa mtu aliyefanya utafiti wa kutosha. Kwani kwa yule anayeamini atakwambia ni kweli na yule asiye amini atakwambia tu sio kweli bila kusema ni kwa
vipi na pengine ni kwa nini.
Tunaposema wanawake wazuri tuna maana pana sana na yenye utata kwa kiasi kikubwa kwa sababu uzuri kama dhana dhahania inachanganya sana.
Je, wanawake wazuri ni wenye sifa zipi na hasa ni wazuri kwa
akina nani na sio kwa wengine? Lakini kwa kusudi lakufikisha ujumbe huu tunaweza kusema wanawake wazuri ni wale ambao watu wengi watu wakiwatazama hukuballi kwamba wana maumbile au sura ambazo zinakubaliwa na maoni yao au maana ya uzuri kwa viwango ambavyo akili zao
zinaamini.
Kuna ukweli wakutosha kwenye dhana hii kwamba wanawake wazuri hupata matatizo au kujijengeamatatizo au vikwazo vya
kuweza kuolewa Kwa nini? Kwanza ni suala la mila na desturi zetu sisi binadamu.Watanzania kama binadamu tunaamini kwamba wanawake wana dhima moja tu hapa duniani. Kumstarehesha mwanaume na pengine kusemwa ni pambo la nyumba.
Mtu anaweza kudhani mawazo haya ni ya jamii kama hizi zetu zilizo nyuma kimaendeleo. Lakini ukweli ni kwamba haya ni mawazo ya karibu dunia nzima hata kwa zile jamii zilizoendelea na ndio maana katika nchi hizo uuzaji wa miili kwa wanawake ni jambo lililopewa baraka na serikali na wana jamii wengi.
Kwa kuwa wanaume wa dunia hii wamelelewa na kujengewa dhana kuwa mwanamke ana kazi kubwa moja tu ambayo ni kumstarehesha mwanaume, humtazama mwanamke kama wanavyo tazama ua au mapambo mengine na huenda mbali zaidi na kumtazama mwanamke kama mashine ya kuwakatia
kiu ya tamaa ya miili yao.
INAKUAJE? Kwa kuwa kwao mwanamke ni mwenye sifa na nafasi hiyo hapa duniani, humtazama mwanamke kwa vipimo
maalumu. Vipimo hivyo ni uzuri wake wa sura kama ilivyo ua na uzuri wa mwili kama ilivyo mashine zifaazozaidi kwa starehe ya kimwili.
Kwa kuwa mwanaume humtazama mwanamke kwa njia hiyo ni wazi pia kwamba humtazama kama kiumbe dhaifu ambaye anahitaji kuhurumiwa, kutunzwa na kuambiwa afanye nini na asifanye kipi kinyume na hayo mwanaume hawezi kamwe kukubali kuwa na mwanamke ambaye ana kauli na anajua kwamba yeye ni mtu kamili na mwenye haki sawa na mwanaume.
Wanaume wengi wanaamini kwamba wanawake wengi wazuri wa sura na maumbile (labda) huwa wana matatizo yakuwaringia wanaume.
Kuwaringia wanaume kuna maana ya mwanamke kutokua tayari kuwa mtumwa wake na kifaa chake cha kukatia kiu ya kimwili.
Kwa imani hiyo wanaume huwa waangalifu sana katika
kushughulika na wanawake wazuri kwani huogopa kwamba watakua wakiteleza pale watakapokuwa wakitaka
kuwabana.
Inawezekana kabisa wanawake wazuri hawana tatizo hilo. Bali wanaume ndivyo wanavyo amini. Kuamini ndiko
kunapopelekea waogope kuwaoa. Wanaume huwa wanasema “mwanamke kama yule hafai kuoa labda kuchezea tu kwani ukimwoa atakusumbua sana…” Kauli kama hii ina maana kwamba mwanamke mzuri ukimwoa atataka kuwa na kauli kwa
sababu ni mzuri nawe itabidi ukubali hili.
Lakini kwa upande wa pili wanawake wazuri naowanapogundua kwamba ni wazuri huku wakiwa wanaamini kwamba uzuri wao ni silaha ya kuwapigia wanaume kamwe hawawezi kuolewa au wanaweza kujikuta ndoa zao hazidumu.
Hii ni kwasababu kwa kuamini kwao hivyo hufanya mambo kwa kiwango cha kupindukia. Huwatenda wanaume yasiyopendeza kwa kuamini kwamba kwa sababu ni wazuri hawawezi kuachwa na hata wakiachwa wataolewa baada ya muda mfupi.
Bili shaka umeshawahi kusikia hata wanawake wenyewe wakisema “flani anautumia uzuri wake vilivyo anawaburuza kweli wanaume” Hii ina maana kwamba uzuri wao ni silaha
nzuri ya kuwashikisha adabu wanaume.
Kwa woga wa kuburuzwa wanaume huogopa kuwafuata wanawake wazuri kwa hiyo unaweza kuona ni kwa vipi wanawake wazuri wanaweza kukosa kuolewa yote inatokana na dhana potofu walizonazo wanaume na hata wanawake kuhusu uzuri na mahusiano
imeandaliwa na Juma Salum
habari zaidi za mahusiano bofya hapa
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA