Jan 9, 2014

ABIRIA WA TREIN INAYOTOKA KIGOMA KWENDA DAR ES SALAAM WAKWAMA MKOANI DODOMA, WAPEWA PESA YA KUJIKIMU


Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubili hatima yao huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.(Picha na John Banda)



 Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na Mzaganza.


Abiria waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuliko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.

 
 Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada train hiyo kukwama kuondoka Dodoma.

 


 Abiria hao wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.

 

CHANZO: PAMOJA BLOG

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA